Kaya Maskini Elfu moja mia nne hamsini na tano ( 1455) zilizoko Halmasahuri ya Wilaya ya Songea ambazo zilikua zikinufaika na Mfuko wa maendeleo ya jamii, TASAF zimehitimu baada ya kunufaika kwa miaka zaidi ya tisa ( 9), wakilipwa fedha na Serikali.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Hosana Ngunge, amewapongeza kaya zilizohitimu kwa kuweza kutumia fedha zao vizuri na kujikuta wameweza kuimalika kiuchumi hivyo kuwaachia wengine nao wanufaike na Fedha hizo ambazo Serikali hutoa kusaidia kaya Maskini.
“ Niwapongeze sana, nimetembelea kaya zenu, nimeona namna ambavyo mmetumia fulsa vizuri kwa kujiendeleza na sasa mmeweza kujitegemea. Ni hatua kubwa na inatia moyo. Kwa hiki mlichofanya sasa mmeweza kuacha nafasi kwa kaya nyingine kuendelea kunufaika kama ambavyo ninyi mmekua mkinufaika.
Nimeona pia wengi wenu mmeweza kuwekeza kwenye ufugaji, nimeona mbuzi, Nguruwe kuku lakini pia nimeona wengine mlikua mnaishi kwenye nyumba za nyasi lakini leo mmeweza kujenga nyumba zenu wenye hili ni jambo kubwa sana mnapasa kumshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nani kama Mama Samia?
Bi Mwana Issa Milanzi ni mmjowa wa waliohitimu baada ya kunufaika kwa miaka kumi tangu 2015, amesema “ Niwashukuru sana TASAF kwa kweli, nilikua nakaa kwenye nyumba ya nyasi inavuja kipindi cha Mvua, ila kwa sasa nimeweza jenga nyumba yangu ya Tofari na nimeweka bati, ninaaman kwa sasa hata mvua inyeshe. Nimeweza kufuga mifugo yangu nina mbuzi watano ambao nilianza kidogo na sasa wamefikia idadi hiyo. Naishukuru sana Serikali imenikwamua.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa