Katibu tawala Wilaya ya Songea Mtela mwampamba amewakumbusha wananchi wa kata ya Muhukuru Lilahi kuwa ardhi ya kijiji haiuzwi na kiongozi yeyote yule.
Mwampamba amesema kuwa Viongozi wa kijiji yaani Halmashauri ya kijiji wanawajibu wa kusimamia ardhi ya kijiji na sio kuuza wala kugawa wenye mamlaka ya kugawa ardhi ya kijiji ni Mkutano mkuu wa kijiji kwa sheria ya ardhi namba nne ya mwaka 1999.
Mtela ameyasema hayo kwenye Hafla ya kuwasha umeme kwenye chuo cha maendeleo ya jamii Muhukuru FDC ambayo imezinduliwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu,sera bunge na uratibu Mhe,Jenista Mhagama.
Aidha Katibu tawala huyo amesema Kumekuwa na Viongozi wa vijiji wanauza ardhi wakati hawana mamlaka ya kuuza wala kugawa ardhi wao ni wasimamizi tu kwa niaba ya wananchi yaani wao ni washenga tu na wala mke sio wao.
Mradi huo ambao umezinduliwa July 16,2024 katika chuo hicho umetumia zaidi ya milioni 100 ni Mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili chini ya wakala wa nishati vijijini REA.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa