Kamati ya siasa ya Wilaya yakagua miradi
Kamati ya siasa ya wilaya ya Songea imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wa Wilaya ya Songea Mh Nelly Duwe pamoja na wajumbe wakamati hiyo walipo tembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea hivi karibuni.
Mh Duwe amesema kamati imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali inavyotekelezwa katika Halmashauri ikiwemo mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Muhukuru, vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kivukoni ambako vimejengwa vyumba sita ,matundu ya vyoo 10 pamoja na ukarabati wa nyumba moja ya mwalimu ujenzi uliogharimu shilingi milioni miamoja na arobaini na moja,mengine ni shule ya msingi Humbaro Kata ya Mpitimbi vimejengwa vyumba viwili ya madrasa na ofisi moja pamoja na madawati 30 ujenzi uliogharimu shilingi miloni 40 kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo.
Aidha amemshauri Mkugurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw Simoni Bulenganija kukabiliana na changamoto zote zinazojijitokeza katika utekelezaji na ukamilishaji wa miradi hiyo ikiwemo changamoto ya mfumo wa malipo ambayo imesababisha baadhi ya miradi kusimama.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Bw Simon Bulenganija amesema atahakikisha atasimamia kazi zote za ujenzi wa miradi na kuhakikisha zinakamilika kwa wakati kabla ya kipindi cha masika kulingana na jiografia ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
JACQUELEN CLAVERY--TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa