Kamati ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma imeridhishwa na utekelezaji wa miradi
Kamati ya siasa ya Makoa wa Ruvuma imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
Mwenyekiti wa ccm wa Mkoa wa Ruvuma ODDO MWISHO ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea uliofanyaki hivi karibuni na kamati ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma .
Mwisho amesema kamati imeridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi hiyo na kuhimiza baadhi ya miradi isiyokamilika ikamilishwe kwa haraka ili wananchi waanze kupata huduma kulingana na huduma iliyolengwa kutolewa katika mradi husika.
Mjumbe wa kamati kuu ya siasa Taifa Mussa Homera ameshauri wataalamu kufanya usimamizi wa pamoja katika utekelezaji wa miradi badala ya kuachia idara husika tu kusimamia mradi.
Wananchi wanaendelea kuishukuru serikali yao kwa utekelezaji wa miradi na upatikanaji wa huduma kwa wepesi na karibu tofauti na awali ambapo walilazimika kufuata huduma hizo kwa umbali mrefu kama vile huduma za Afya, Elimu na huduma nyingine za kijamii.
Kamati hiyo ilifanikiwa kutembelea Zahanati ya Lugagara kata ya Kilagano, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Litapwasi kata ya Litapwa ambavyo vimekamilika kwa asilimia mia moja na vimeanza kutumika ,ujenzi wa Hospitali ya Wilaya inayojengwa katika kijiji cha Mpitimbi (B) kata ya Mpitimbi ambao umekamilika kwa asilimia 85 miradi mingine ni kituo cha Afya Muhukulu Lilahi ambacho kimekamilika kwa asilimia 90, Chuo cha maendeleo ya Wananchi Muhukulu na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa vya shule shikizi ya Maleta kata ya Ndongosi.
JACQUELEN CLAVERY-K/AFISA HABARI.
SONGEA DC
20 /08 /2019.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa