KAMATI ya Siasa Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Ndugu Mohamed Ally imefanya ziara ya Ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Ukaguzi huo umefanyika katika Kata ya Parangu ambapo kuna ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa, vyoo matundu 20 na mabweni manne 4 katika Shule ya Sekondari Jenista Mhagama.
Mradi huo unatekelezwa na fedha kiasi cha shilingi Milioni 834 kutoka Serikali Kuu na Milioni 128 kutoka SEQUIP.
Vilevile Kamati ya Siasa Mkoa imekagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Lugagara Kata ya Kilagano unaotekelezwa na fedha kiasi cha shilingi milioni 560 kutoka Serikali Kuu.
Mradi huu unategemewa kukamilika mwaka huu kwaajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2024 ambapo utasaidia kupunguza utoro kwani kabla wanafunzi walikuwa wakitembea umbali mrefu kwenda sekondari ya Kilagano.
Na mwisho kamati ya Siasa Mkoa imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya Nambarapi iliyopo Kata ya Kilagano unaotekelezwa kwa fedha kiasi cha shilingi Milioni 331.6 kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa BOOST.
Akizungumza katika ziara hiyo Ndugu Mohamedi Ally amewataka mafundi Viongozi kuongeza kasi ili miradi ikamilike mapema na iweze kutumika.
Aidha, Kamati ya Siasa imeridhishwa na miradi yote waliyoitembelea na wamepongeza Timu ya wataalamu ya Halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi Ndugu Neema, Baraza la Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Menas Komba na Viongozi wa Chama wakiongozwa na Mhe. Thomas Masolwa kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo kwani thamani ya fedha inaonekana katika miradi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa