Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea imefanya ziara ya siku mbili kuanzi tarehe 31/08/2023 hadi tarehe 01/08/2023 katika miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa ndani ya Halmashauri. Kamati hiyo iliongozwa na Mh. Menas Komba ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Katika ziara hiyo, kamati iliweza kutembelea jumla ya miradi saba 7 ikiwa ni pamoja na shule ya Sekondari Jenista Mhagama, nyumba ya mtumishi Zahanati ya Mdunduwalo, Chuo cha Walemavu Liganga, Zahanati ya Mpitimbi “A” Nyumba mbili za watumishi Hospitali ya Wilaya Mtipimbi , soko la kimkakati la Matomondo na Nyumba mbili za watumishi kituo cha Afya Magagura.
Kamati ikiwa katika Shule Sekondari ya Jenista Mhagama,Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo alisoma taarifa na katika taarifa yake, alikiri Shule ilipokea kiasi cha pesa kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali “ tumepokea shilingi 800,000,000, kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa matundu 20 ya vyoo, Mabweni 4na madarasa 12.” Mafundi wote wanamkataba wa miezi mitatu na wote wapo ndani ya muda alisema mkuu wa shule.
Kamati pia ilitembelea Zahanati ya Mdunduwalo, kufanya ukaguzi wa nyumba moja ya watumishi wa Zahanati hiyo, ambayo ni moja kwa mbili ( two in one). Mradi ambao unafadhiliwa na Tanzania Social Action Fund (TASAF), akiwasilisha taarifa hiyo, mtendaji wa kijiji alisema “ tumepokea fedha kiasi cha TZS 154,000,000. Kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa nyumba ya watumishi, vyoo na kuchimba kisima cha maji. Ambapo mpaka sasa ujenzi unaendelea vizuri, vifaa vyote vipo, na mafundi wapo ndani ya muda wa mkataba waliopewa.
Serikali kupitia ofisi Kuu, imeanzisha ujenzi wa chuo cha Walemavu, kilichopo kata ya Liganga, katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea hivyo, Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango pia ilifika kata ya Liganga kujua mwenendo wa Ujenzi huo. Mwenyekiti na kiongozi wa msafara Mh. Menans Komba,alimtaka Mtendaji wa Kata hiyo kuihabarisha kamati mwenendo wa Mradi huo. Ambapo msemaji wa kata hiyo alisema “ Mradi huu ulianza tarehe 19/05/2023, baada kupokea Fedha kiasi chaTZS 1,007000,000 kutoka Serikali kuu na awali tulianza na Ujenzi wa ;-
i. Stoo ya vifaa
ii. Ujenzi wa hostel
iii. Madarasa 10
iiii. Nyumba za watumishi
Japo Mh. Mwenyekiti, tulikua na changamoto ya maji, ila tumeshawasilina na RUWASA, wanaangalia namna ya kutusaidia, ili kufikisha maji kwa urahisi.
Serikali pia kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa kuzingatia umuhimu wa huduma ya afya, imejikita katika ujenzi wa miundombinu katika Zahanati na Vituo vya Afya ili kuwawezesha wananchi wake kupata huduma bora na karibu na mazingira yao hivyo, kata na vijiji tofauti vimekua vikiwekewa pesa kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo.
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango iliona ni vyema pia kupita na kukagua miradi hiyo katika Hospitali, Zahanati na Vituo vya Afya, ili kujiridhisha pasipo shaka kwamba pesa inayotoka na Serikali inatumika kama ilivyoagizwa. Hivyo kamati ilianza na Zahanati ya Mpitimbi “A” ambapo Serikaliilitoa Shilingi 50,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati, hivyo kulingana na maelezo ya mtendaji wa Kata, Pesa hiyo ilikua ni kwa sababu ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati pamoja na vyoo. Ambapo mafundi wanaendelea na kazi, na mpaka mwezi wa Nane, kila kitu kitakua tayari na Zahanati itaanza kutumika.
Hospitali ya Wilaya, Halmshauri ya Wilaya ya Songea, iliyopo Mpitimbi. Serikali imetoa pesa kwa ajili ya Ujenzi wa nyumba mbili za watumishi kupitia taarifa iliyowasiishwa na Kaimu Mtendaji wa Kata ambapo alisema “ tumepokea Shilingi 120,000,000 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa nyumba mbili za watumishi, mradi huo ni kwa kipindi cha miezi mitatu kwanzia Mei mpaka Julai. Jumla ya shilingi 74,000,000 zimeshatumika, na tumebaki na shilingi 46,000,000 na mradi upo 80%.
Nyumba mbili za watumishi Kituo cha Afya Magagura, ni sehemu ambayo kamati pia ilitembelea na Mtendaji wa Kata alisema “ mradi huu tulipokea jumla ya shilingi 120,000,000 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi kwa kipindi cha miezi mitatu, Mei mpaka Julai. Na kufikia hapa mradi unaenda vizuri, kulikua na changamoto kidogo, ila tunawashukuru viongozi wetu, kila kitu sasa kinaenda vizuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ipo kwenye muendelezo wa Ujenzi wa Soko la kimkakati la Matomondo, soko ambalo litasaidia wakazi wa maeneo haya kupata huduma kwa ukaribu na urahisi huku pia Halmashauri ikiingiza kipato kupitia Soko hilo. Ambapo Mh. Mwenyekiti, wakati cha ziara aliagiza kuwe na mpango mkakati katika usimamizi wa ujenzi wa soko hilo la Kimkakati ili kuhakikisha linakamilika kwa wakati sahihi.
Viongozi wa kata, na wenyeviti kwa Niaba ya wananchi wao, Waliwashukuru viongozi wa Serikali na viongozi wa Chama, Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo Mh. Jenista Mhagama, Mwenyeiti wa balaza la madiwani pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa jitihada walizonazo katika kuwasaidia wananchi wao, kwa kuweka miundombinu vizuri lakini pia kuisimamia ili iweze kuisha kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa