JAMII tunzeni siri za,tamaduni,mila na desturi za makabila
Kauli hiyo ameisema Romward Shawa mzee maarufu wa kabila la wangoni anayeishi katika kata ya Maposeni kijiji cha Maposeni mtaa wa Ndilima.
Mzee Shawa amesema jamii itunze siri za mila,tamaduni na desturi za makabila ili kulinda maadili na kujiepusha na madhara yanayosababishwa na ukiukaji wa maadili katika jamii kama vile mimba za utotoni,ongezeko la watoto wanaishi katika mazingira magumu,magonjwa uvunjifu wa amani hata vifo.
Amesema watoto wanatakiwa kupewa mafunzo ya stadi za maisha pale wanapotakiwa kupewa mafunzo hayo,kupatiwa mafunzo katika umri ambao haustahili ni sawa na ukiukaji wa maadili na kusababisha madhara kwa jamii inayo husika.
Bi Teodosia Komba anatoa ushauri kwa jamii kuendelea kudumisha mila na desturi zetu ambazo zinalinda maadili ya nchi na kusoma historia za vizazi vilivyotangulia ili wananchi wajue mila tamaduni na desturi za makabila yao mfano kabila la wangoni moja ya mila yake ni wanawake na wanaume kuishi mazingira tofauti akinamama uani na akinababa kibarazani hata kwenye upande wa kuzikwa.
Amesema swala la utandawazi likitumika kwa makusudi yalikusudiwa halina madhara kwasababu unasaidia kutuelimisha na sio lazima kuiga mila na tamaduni za kigeni ambazo zinavunja maadili ya Kitanzania.
Bw Shawa amesema jamii iendeleze mila na desturi ambazo zinajenga maadili mazuri ambayo yanasaidia kudumisha amani, upendo na mshikamano kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa, Jambo ambalo linaleta utengamano na kuondoa migogoro pamoja na kujenga kizazi chenye heshima.
Bw Shawa amesema jamii iendeleze mila na desturi ambazo zinajenga maadili mazuri ambayo yanasaidia kudumisha amani, upendo na mshikamano kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa, Jambo ambalo linaleta utengamano na kuondoa migogoro pamoja na kujenga kizazi chenye heshima.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa