Jamii imeshuriwa kuchukua tahadhari na kuzingatia kanuni taratibu na sheria inayozuia kula mizoga au nyama isiyokaguliwa na wataalam wa mifugo ili kijikinga na magonjwa ya milipuko na kuepuka gharama za kutibu magonjwa hayo
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dr Erick Kahise hivi karibuni ofisini kwake
Dr Kahise amesema kutozingtia sheria kanuni na taratibu ni chanzo cha kupata magonjwa ya milipuko na kusambaa kwa magonjwa hayo katika jamii mbayo yanatoka kwa Wanyama kwenda kwa binadamu.
Dr Kahise ametaja mfano wa magonjwa ambayo yanaweza kulipuka kuwa ni minyoo ya nguruwe ambayo hukaa ndani ya ubongo kwa muda mrefu na kusababisha kifafa,kutupa mimba kwa ng’ombe ambao binadamu anaweza kupata na dalili zake zinafanana na za malaria,kunywa maziwa mabicha ambayo yametokana na ngonmbe mwenye vimelea vya TB (micobacterium bovis).
Ameongeza kwakusema kuishi na wanyama ndani ya nyumba moja na kuacha mifugo kuzurula ovyo kama mbwa ni hatari kwa afya ya binadamu kwasababu nao husambaza magojwa kama kichaa cha mbwa ambacho kinaonekana kuwa tishio kwa uhai na ustawi wa binadamu utitiri ,viroboto na chawa ambayo husambazwa na kuku.
“Jamii ibadilike panapotokea tatizo la ugonjwa kwa mnyama naakafa waache kukimbilia kula nyama bali watoea taarifa kwa mamlaka husika ili taratibu zakitaalam ziwezekufanyika”,amesema Dr Kahise
Dr kahise ametaja mikakati ya kudhibiti magonjwa hayo nipamoja na watu wote wanao husika na uchinjaji na uuzaji wa nyama wanachinje maeneo rasmi yaliyo ruhusiwa na Serikali,kudhibiti kwakuchanja mifugo ,sambamba na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kukinga ya mifugo ambao tayari umeanza kutekelezwa katika kata ya Peramiho,Kilagano na Ndongosi.
Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Dr.Jofrey Kihaule amesema katika klpindi cha mwaka 2019 hadi Oktoba 2020 jumla ya watu 340 waliung’atwa na mbu kati ya hao watu 20 walithibitika kuugua kichaa cha ,mbwa.
Shilika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) limeitaja Nchi ya Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazo kabiliwa na tatizo la magonjwa ya milipuko yanayo toka kwa Wanyama kwenda kwa binadamu,sababu ikitajwa mwingiliano wa Wanyama na binadamu kutoka eneo moja kwenda jingine ndani na Nje ya Nchi.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari, Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa