Baada ya mapumziko ya mwezi mzima (Siku thelathini ) wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, sasa wamefungua Shule rasmi leo tarehe 1/07/2024 na kuanza masomo yao kama ratiba ya Shule ilivyopangwa.
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, wamekiri kupokea idadi kubwa ya Wanafunzi ambao leo wameingia Shuleni, wakiwa wako vizuri na wamejiandaa kwa ajili ya kuanza masomo yao.
Akizungumza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Peramiho Mwl. Maskalina Ngonyani amesema “ Tunashukuru wanafunzi leo wamefika kwa wingi, tena wakiwa na morali ya kusoma, lakini pia Walimu wamekua wakipishana Madarasani kwa ajili ya kuhakikisha wananfunzi leo wanasoma kama kawaida.
Aidha Walimu wameendelea na vipindi kama kawaida, hivyo kuwafanya wanafunzi kujiweka sawa kiakili na kimwili kwa ajili ya Masomo.
hata hivyo wadau wengi wamepongea kwa namna Walimu walivyoanza kwa kasi ili kukimbizana na muda na hata hivyo itasaidia kumaliza topik kwa wakati ili waweze kupata muda wa kutosha wa kufanya marudio kwa maeneo ambayo hayakueleweka vemao.
Wazazi na walezi pia wameendelea kuleta vyakula kwa ajili ya watoto kipata chakjla vha mchana kama walivyokubaliana. Watoto wote wanapaswa kipata chakula cha Mchana
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa