Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Kapenjama Ndile jana terehe 07/02/2024 alikutana na Wakuu wa Shule zote za Msingi na Sekondari wa Halmashauri ya Songea ili kupata Taarifa ya uandikishaji na uripoti wa wanafunzi wa Darasa la Awali, Darasa la kwanza na Kidato cha kwanza 2024 .
Aidha Mkuu wa Wilaya alipongeza jitihada zinazofanywa na wakuu wa Shule ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji uliopelekea kuongeza idadi ya wanafunzi wa darasa la Awali, Kidato cha kwanza na Darasa la kwanza ukilinganisha na hali ilivyokua katika kikao kazi cha tarehe 17/01/2024.
Mhe. Ndile ameyasema hayo kwenye kikao cha wakuu wa shule watendaji wa vijiji na kata na maafisa elimu wa kata kilichofanyika katika ukumbi wa Jenista Mhagama uliopo Shule ya Sekondari Maposeni. Pamoja na wadau wengine wa Elimu, Mkuu wa Wilaya aliambatata na Katibu tawala wa Wilaya Mr. Mtela Mwampamba, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mwl. Neema Maghembe pamoja na Maafisa Elimu Msingi na Sekondari
“Lengo la Halmashauri kwa mwaka 2024, ni kuhakikisha watoto wote walioandikishwa kuanza Elimu ya Awali 3946 na Darasa la kwanza 4123 wanaandikishwa kwa asilimia 100. Aidha kwa upande wa Sekondari, Halmashauri itahakikisha wanafunzi wote 2605 waliofaulu na kupangiwa shule za Kata wanaripoti kwa asilimia 100”
Uandikishaji kwa mwaka 2024 umeanza na unaendelea vizuri kwani hadi sasa jumla ya wanafunzi wa Awali 4609 ambao ni sawa na asilimia 93% wameandikishwa shule na wanafunzi 4587 wa darasa la kwanza ambao ni sawa na asilimia 94% ya waliotarajiwa wameandikishwa.
Aidha jumla ya wanafunzi 4480 wa darasa la Awali na ambao ni sawa na asilimia 97% na wanafunzi 4536 wa darasa la kwanza sawa na asilimia 99 ya walioandikishwa wameripoti Shulen na wanaendelea na masomo
Kwa upande wa shule za sekondari,jumla ya wanafunzi 2117 sawa na asilimia 81 wameripoti shuleni na wanaendelea na masomo huku juhudi zaidi zinaendelea kufanyika ili kuhamasisha wazazi/walezi kupeleka watoto shuleni. Sambamba na kuwafuata wanafunzi waliofaulu nyumba kwa nyumba ilikujiunga na shule
Katibu tawala wa Wilaya ya Songea, Mtela Mwampamba asisitiza mambo mawili:- wanafunzi wote wenye sifa na waliofaulu kuingia kidato cha kwanza, wafike mashuleni Wazazi na walezi wahakikishe wanawaepusha watoto ( wanafunzi) na ajira za mashambani, kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wao na kuwakosesha haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Ikumbukwe kwamba, Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan inatoa Elimu bure kwanzia Awali, Msingi na Sekondari
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa