Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Kapenjama Ndile amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kukaa tayari kuupokea uwekezaji wa kiwanda kikubwa cha sukari katika Kata ya Lilyai Kijiji cha Magwamila.
Ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao na wataalamu wa ardhi wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea, wataalamu wa bodi ya sukari Tanzania na wawekezaji wenyewe kutoka Madwani Group kilichofanyika Leo 09.01.2024 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea. Ambapo Kapenjama Ndile ameeleza kwamba,
"Songea Sukari ni kiwanda kitakachojengwa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Kata ya Lilyai Kijiji cha Magwamila hivyo Leo tunafanya mapitio ya maombi ya wawekezaji ambapo wao wanatarajia kuweka zaidi ya Bilioni 500 katika kiwanda hicho, ambapo kiwanda kitazalisha Tani zaidi ya laki moja kwa mwaka, pia kitaweza kuzalisha umeme ambao utaweza kuuzwa kwenye grid ya Taifa, pia kitazalisha mafuta aina ya ethane hivyo kuwepo kwa kiwanda hicho kitaleta manufaa makubwa sana katika Halmashuri yetu hivyo nitoe wito kwa wananchi wa Wilaya ya Songea hususani Songea vijijini kupokea mradi huu kwa mikono miwili".
"Nae Mchumi mwandamizi wa Bodi ya Sukari Tanzania Joshua Mhando amesema " kwa ujimla Bodi ya Sukari Tanzania inashukuru sana kwa mchakato mzima unaondelea hapa Halmashuri ya Wilaya ya Songea kwani kwetu sisi tunapendezwa sana na uwekezaji wa uzalishaji wa sukari katika nchi yetu pia tunawashukuru sana wawekezaji kwa kuweka Nia ya kuwekeza katika Wilaya hii, hivyo napenda kuishukuru sana Serikali chini Raisi wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji nasi tunamuahidi kutoa ushirikiano ili kuleta maendeleo katika Taifa letu"
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Ndg Makisio Chengula amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Songea kwaajili ya kikao hicho cha mapitio hayo ya maombi ya uwekezaji katika Halmashuri ya Wilaya ya Songea kwani kupitia wawekezaji hao Halmashauri itaweza kuingiza fedha nyingi kama mapato, pia amemshukuru Mhe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika nchi yetu hususani katika Halmashuri ya Wilaya ya Songea.
Pia mjumbe wa Madwani Group ( mwekezaji) Kapil Dave amemshukuru kwa mapokezi mazuri waliyoyapata na kuwezesha kikao hicho kufanywa kwa amani, pia ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuweka utaratibu mzuri wa uwekezaji katika nchi hii na amesema iwapo watapewa nafasi ya kuwekeza katika eneo hilo la Magwamila basi ameahidi kufanya uzalishaji wenye tija na wenye kuleta maendeleo chanya katika jamii na nchi kwa ujumla.
Eneo la uwekezaji linatarajiwa kuwa na ukubwa wa hekta elfu 30 ambapo hekta elfu 22 zitakuwa kwaajili ya Kilimo cha miwa na hekta elfu 8 kwaajili ya huduma nyingine ikiwa ni pamoja na ufungaji wa mitambo (kiwanda), barabara za ndani, maghara, makazi ya watumishi ( vibarua ) ujenzi wa huduma za kijamii ikiwemo shule pamoja vituo vya afya. Sambamba na hilo wananchi watapewa hekta elfu 14 kwaajili ya kilimo cha miwa ambayo wataiuza katika kiwanda hicho ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa