Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Chirstina Mndeme amesema Mkoa umejipanga vizuri katika kuhakikisha Watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2021 wanaanza kidato cha kwanza bila vikwazo vyovyote.
Mndeme ametoa kauli hiyo kwenye kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mndeme amesema Mkoa wa Ruvuma umejipanga vizuri katika swala zima kuhakikisha watoto wote walio chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaanza masomo bila kikwazo kwasababu miundo mbinu ya kufundishia na kujifunzia ipo na inakidhi mahitaji.
“Tunahitaji jitihada za pamoja kuongeza ufaulu”,amesema Mndeme.
Akiongelea kuhusu ufaulu Mndeme amesema mwaka 2020 ufaulu ni asilimia78.52 na umeshuka kwa asilimia 5.12 ukilinganisha na mwaka 2019 ufaulu ulikuwa asilimia 83.70 kwa wanafunzi wa darasa la saba hivyo zinahitajika jitihada za pamoja ili kuongeza ufalu katika Halmashauri zote.
Ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Songea kushika nafasi ya kwanza Kimkoa kwa kufaulisha kwa asilimia 85.51 huku akiitaka Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuongeza jitahada za kufaulisha kwani imekuwa ya mwisho, na imefaulisha kwa asilimia 66.8 kinyume na lengo la Mkoa la kufaulisha kwa asilimia 90.
Mndeme amewapongeza walimu wa shule za sekondari kwa kufaulisha wanafunzi wa kidato cha sita kwa asilimia 98.8 mwaka 2020.
Ametoa wito kwa kamati ya ushauri ya Mkoa kushirikiana kwa pamoja kujenga shule ya wasichana katika Halmashauri ya Madaba ambayo itachukua wanafunzi kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwanusuru watoto wa kike na vikwanzo ambavyo vinakwamisha jitihada zao za kusonga mbelea na masomo.
Baadhi ya wazazi na walezi wamezidi kuipongeza serikali kwa mpango wa Elimu bure,mpango ambao umewasaidia kuwapeleka Watoto wao shule kwa wakati na Watoto wote wanaostahili kwenda shule na kuto wapangia majukumu ambayo si yao kama vile kuchunga mifugo na kuchuuza bidhaa.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery-Kitengo cha Habari
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa