Afisa nyuki kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea David Kikasi leo ameendesha mafunzo katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea ya ufugaji bora wa nyuki kwa kikundi cha HAPA KAZI TU kutoka peramiho.
Akitoa mafunzo hayo amekipongeza kikundi hicho kwa hatua waliyoifikia mpaka sasa kwani wameweza kumiliki mizinga 32 richa ya kuwa na elimu ndogo ya ufugaji wa nyuki. Amesema
“Kwa sasa ufugaji wa nyuki unafaida kubwa sana katika kukuza uchumi wa jamii zetu hivyo niwapongeze kwa hatua mliyofikia mpaka sasa naamini kupitia elimu ya leo mtaenda kuongeza kipato chenu kupitia mazao ya nyuki kwa maana kwa hali ya sasa kilo moja ya asali ya nyuki inauzwa shilingi 10,000”
Kisha elimu hiyo iliendelea kutolewa kwa kutazama aina za nyuki na mazao yanayopatikana kupitia ufugaji wa nyuki ambapo amesema.
“Kwa kuanza tutazame aina za nyuki ambao wanapatikana katika mzinga au msafara wa nyuki ambapo kuna aina tatu za nyuki nao ni nyuki dume hawa wanakuwa 200 mpaka 400 katika kundi moja nao kazi yao ni kumpanda malkia tu , pia kuna nyuki malkia ambapo kwenye kundi anakuwa ni mmoja tu, na aina ya tatu ni nyuki vibarua ambao kazi yao ni kwenda kutafuta chakula”.
Na mazao yanayotokana na kilimo cha nyuki ni pamoja na asali ambayo kila mmoja anaifahamu kutokana na utamu wake pia zao lingine ni nta ambayo hutumika kutengenezea sabuni, mafuta ya kupaka, mishumaa nk, zao lingine ni chavua/ sinde huu ni ungaunga unaopatikana kwenye maua nyuki hubeba kwenye mabawa nao unavunwa kwa kifaa maalumu husaidia sana kwa wenye matatizo ya macho, kisukali, pia kuna mkate wa nyuki, kuna sumu ya nyuki ambayo bado ipo kwenye utafiti ambayo inasemekana inawea kutibu kansa, pia kuna zao linaitwa chakula cha malkia (royal jerry) ambayo huondoa hali ya ngozi kuzeeka
Nae mwenyekiti wa kikundi cha HAPA KAZI TU Ksavel Haule amemshukuru Afisa nyuki wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa kuwapatia elimu juu ya ufugaji bora wa nyuki na kusema kwamba kupitia elimu hiyo itakwenda kuwanufaisha kwa kupata mazao yenye tija na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kikundi kwa ujuml
a.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa