Dkt. Samia Suluhu Hassan amaliza ziara yake leo 28.09.2024, ambapo alifanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya Majimaji vilivyopo Mkoani Ruvuma
“Nawashukuru sana wanaRuvuma, nimepata mapokezi makubwa katika kila eneo nililoyembelea, wananchi walikuja kwa wingi na furaha sana, wamenipa zawadi nyingi sana hii ni kuashirilia kwamba wanatambua jitihada zetu za kuboresha maisha na ustawi wao” amesema Dkt. Samia
Wakati akizungumzia Wilaya alizotembelea ndani ya Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Rais aliongelea ziara yake ambayo alitembelea Shamba la Kahawa la Aviv lililoko halmashauri ya Wilaya ya Songea, na kueleza jitihada za Serikali katika kutoa Mbolea ya Ruzuku kwa Wananchi wa Ruvuma
“Nilipata fursa ya kukagua shughuli za Kilimo cha Kahawa kwenye shamba la Aviv, kwakua Ruvuma ni wakulima wazuri sana nataka nielezee jitihada zinazofanywa na Serikali kwenye Sekta ya kilimo katika mkoa huu.
Serikali imetoa ruzuku ya Mbolea yenye thamani ya Tsh. Bilion 83.5”
Aidha Dkt. Samia ameitaja barabara ya Likuyufusi hadi Mkenda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea yenye urefu wa kilomita 60 itakayokwenda kutuunganisha na Msumbiji, akisema kwamba mkandarasi atapatikana mwezi wa kumi na shughuli za ujenzi zitaendelea.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa