Halmashauri ya Wilaya ya Songea imeendelea kutekeleza hatua za Lishe kwa kufuata mwongozo wa Taifa wa Lishe pamoja na sera mbalimbali za nchi zinazolenga kuzuia na kupambana na Udumavu na Utapiamlo mkali kwa watoto chini ya miaka mitano.
Katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/224 Halmashauri ya Wilaya ya Songea imefanya shughuli za usimamizi elekezi ambazo ni kuangalia utoaji wa Elimu ya Lishe katika vituo vya kutolea Huduma za Afya, Utambuzi na Matibabu ya Utapiamlo Mkali na Upimaji wa hali ya Lishe kwa Watoto wa chini ya miaka Mitano.
Sanjari na hayo, umefanyika pia uhamasishaji wa utoaji wa chakula shuleni kupitia mikutano ya Hadhara iliyoendeshwa na watendaji wa vijiji na Kata ambapo wazazi walielezwa faida za wanafunzi kupata chakula shuleni na jinsi itakavyosaidia kupunguza utoro, uachaji shule na namna itakavyosaidia kukuza kiwango cha ufaufalu kwa wanafunzi.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Afua za mkataba wa lishe robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024 Afisa Lishe wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Bi. Joyce Sipira Katika kikao cha Lishe kilichofanyika tarehe 25 Oktoba 2023 ameeleza faida za lishe Bora na hasara za lishe duni katika mwili ambapo amesema
" Lishe Bora ni ulaji wa chakula cha kutosha, vizuri pamoja na shughuli za kawaida za kimwili ni jiwe la Msingi la afya njema, pia ni muhimu kwa afya njema ya ajili na mwili, lishe Bora imebeba viini lishe ( virutubisho ) vilivyoko kwenye chakula ambavyo husaidia kujenga na kuuwezesha mwili kufanya kazi zake vizuri na kila kirutubisho kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi zake kwa ufanisi. Lakini tunapozungumzia lishe duni inaweza kusababisha Kinga kupungua, kuongezeka kwa uwezekano wa kupata magonjwa, kuharibika mwili na kuathiri maendeleo ya ajili na ufanisi wa uzalishaji.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Wilman Kapenjama Ndile ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa kikao cha uwasilishaji wa taarifa hiyo amesema " watu wahimizwe kula vitu vya asili ambavyo vinapatikana maeneo waliyopo ili kujenga afya Bora ya miili yao kuliko kutegemea kula samaki tu tena wanatoka mbali, kikubwa tuangalie wadudu gani wanalika kwa ukanda wetu na wanapatikana wakati gani kwa wingi kwa kufanya hivyo tutaepukana na lishe duni kwa watoto wetu na wananchi kwa ujumla na hata kama kuna watu wanakula panya basi Elimu itolewe watiwe moyo kwamaana nao ni wadudu ambao wanaprotini kuliko kuwasema watu wanaokula hao panya na pia waambiwe ni panya gani ndio wanaliwa hususani wale wa porini".
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa