MKUU wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Wilman Kapenjama Ndile akiwa na wakuu wa Idara na Vitengo amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata ya Liganga na Kilagano.
Miradi iliyotembelewa ni Pamoja na mradi wa ujenzi wa Chuo cha walemavu kinachojengwa katika Kata ya Liganga ambapo Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha shilingi Bilioni Moja kutoka Serikali Kuu.
Vilevile DC Ndile amekagua ujenzi wa mradi wa BOOST wa madarasa Matano na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Mbolongo ambapo walipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 125,100,000/= kutekeleza mradi huo.
Pia amefanya ukaguzi wa mradi wa SWASH unaotekelezwa katika Kata ya Kilagano ambapo kuna ujenzi wa matundu 13 ya vyoo katika shule ya msingi Mhimbasi ambapo walipokea fedha kiasi cha Shilingi milioni 34.2 kutekeleza mradi huu.
Akizungumza katika ukaguzi huo amewataka mafundi kuandaa mpango kazi na kuufuata ili kuhakikisha miradi inakamilika kabla au ifikapo Juni 30 2023 ikiwa katika ubora na viwango vinavyokubaliwa na Serikali.
Vilevile amewataka Walimu kuwasaidia Walimu wakuu katika usimamizi wa miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika mapema.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa