CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.
Wananchi wametakiwa kutambua chanjo dhidi ya ugonjwa wa saratani y mlango wa kizazi nichanjo salama na haina madhara yoyote kwa watoto wakike
Hayo yamesemwa na wataalam mbalimbali wa afya katika zoezi la uzinduzi wachanjo ya saratani ya mlango wa kizazi uliofanyika katika shule ya Sekondari Maposeni Mji mdogo wa Peramiho.
Wataalam hao wamesema chanjo hiyo ni salama na haina madhara kwakuwa imethibitishwa na shirika la Afya duniani na Mamlaka ya chakula na dawa nchini hivyo wananchi waondoe hofu kwa watoto wao watakao patiwa chanjo hiyo.
Mganga mkuu wa wilaya ya Songea Dr Yesaya Mwasubira amesema chanjo hiyo imefanyiwa majaribio katika Mkoa wa Kilimanjaro na kutoa mafanikio makubwa.
Amesema chanjo zote zinazotolewa dhidi ya magonjwa zina faida nyingi kama kuepukana na magonjwa,kupunguza vifo katika jamii na kujengaTaifa la watu wenye afya bora .
Amesema walengwa wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ni wasichana wato wenye umri wa miaka kumi na nne (14) mwaka 2018 na mwaka 2019 wataanza kuchanja wasichana wenye umri wamiaka 9,wameanza kuchanja kundi hilo kwasababu kundi ambalo linakaribia kujihusisha na mapenzi. chanjo hiyo hutolewa bure na endelevu kama chanjo nyingine zinazotolewa
Adha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Bw Simon Bulengenije ametoa wito kwa wananchi kuwa waruhusu watoto wao kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili waweze kuepukana na maambukizi ya virusi vinavyo sababisha ugonjwa huo ambao hauna tiba dhidi yakujikinga tu.
Amewataka wahudumu wanao husika na zoezi la utoaji wa chanjo kuwafikia walengwa wote hata wale wasio kuwa mashuleni katikaHalmashauri na kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara makubwa yatokanayo na ugonjwa wa saratani kwa familia,jamii,na Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh Pololeti Mgema ametoa onyo kwa mtu yeyote atakaye thubutu kuhujumu zoezi la uchanjaji wa chanjo mpya ya saratani ya mlango wa kizazi atachukuliwa hatua za kisheria bila kujali wadhifa wake na kuendelea kuunga mkonojitihada za serikali katika kuhamasisha maendeleo.
Ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ni ugonjwa unaongoza kusababisha vifo kwa wanawake wengi kwa asilimia 50 ukilinganisha na magonjwa mengine. Dalili zake kutokwa damu bila mpangilio au baada ya kujamiina,maumivu ya mgongo,miguu,na kiuno,kuchoka,kupungua uzito,kukosa hamu ya chakula na kutokwa uchafu kwenye uke wa majimaji,uliopauka wa rangi ya kahawia au wenye damu.
Na husababishwa na kuanza kujamiiana katika umri mdogo,kuwa nawapenzi wengi, ndoa za mitala,kuzaa watoto wengi nauvutaji wa sigara.
Halmashauri ya wilaya ya Songea inatarajia kutoa chanjo kwa mabinti zaidi ya 2000 .
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa