HALMASHAURI ya wilaya ya songea imevuka lengo la kuchanja kwa asilimia 124 ya chanjo ya polio ambayo inazuia ugonjwa wa kupooza hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambao walipangwa kufikiwa.
Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dr.Geofrey Kihaule amesema kupitia zoezi la kampeni maalum ya kuthibiti maambukuzi ya ugonjwa wa POLIO imefanikiwa kuchanja watoto 37,205 ambao walilengwa kufikiwa kupitia kampeni hiyo.
Dr Kihaule ametaja sababu ya kuendesha zoezi la kampeni ni kuimarisha kinga hasa kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Dr. Kihaule ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwapeleka watoto katika vituo vya kutolea huduma iliwaweze kupatiwa chanjo kwasababu zoezi la utoaji wa chanjo ya polio na chanjo nyingine ni endelevu licha ya siku zilizopangwa kumalizika.
Chanjo ya polio ni chanjo inayotolewa kwa watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi miaka mitano ambayo inazuia ugonjwa wa kupooza hasa kwa watoto wadogo wenye umri huo.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Septemba 07, 2022.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa