Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofice ya Waziri Mkuu( Sera Bunge na Uratibu) aagiza Bwawa la maji lililopo Mpitimbi lenye ukubwa wa km 17 liingizwe kwenye mpango wa kurekebishwa ili nalo lianze kufugwa samaki kwa ajili ya kuendelea mradi wa viumbe maji Songea.
Waziri aliyasema hayo baada ya Mwenyekiti wa Halmashaurinya Wilaya ya Songea, Mhe. Menans Komba kutoa hoja katika uzinduzi wa Kuendeleza Lishe na Ufugaji endelevu wa Viumbe maji kwa Wakulima wadogo jana katika mabwawa ya Samaki Mpitimbi.
“ Mhe Waziri, pamoja na viongozi mliambatana nae, kuna bwawa la Mungu lipo hapa hapa mpitimbi tena lipo njiani tu hapo ambapo mnaweza pita nakujionea ili kuangalia namna mnaweza kulitumia bwawa hilo ambalo ni kubwa na linauwezo wa kuingia samaki wengi kama litatengenezwa vizuri, litasafiswa linaweza kusaidia mradi huu wa samaki ambao Serikali ya Rais Samia umeuwekea nguvu na kusaidia wananchi wa Songea.
Aidha ili kuonesha kwamba ombi hilo ni muhimu kwa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mhe. Komba alipiga goti kwa Mhe. Jenista Mhagama, Ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho. Ndipo Mhe. Mbunge aliona atoe tamko papo hapo kwa viongozi na wananchi kuwa wamelipokea jambo hilo na wameanza kulijadili papo hapo ili kuangalia namna ya kulimaliza.
Akizungumza baada ya kupokea ombi hilo mhe. Jenista Alisema “Kaka yangu Menans Komba, umeweka Hoja nzito, hoja hii ni hoja ya Mbunge wako pia, wananchi wa Mpitimbi tunalo bwawa la asili hapa mpitimbi kupitia mradi huu nji wakati muafaka sasa bwawa lile lijengwe liimarishwe na Ufugaji wa samaki mkubwa uanze”
Lakini pia Mhe Mwenyekiti alimshukuru Mhe. Mbunge kwa namna anavyochukua changamoto za wananchi na kuzifanyia kazi, aidha alimshukuru pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Sukuhu Hassan kwa kuweka Rasilimali fedha kwenye Miradi ya Mifugo na Uvuvi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa