Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), Julai 31, 2024 amekagua Uwanja wa Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nane Nane 2024 na kuelekeza kuwa ni tayari kuanza rasmi leo Agosti 1, 2024 katika Kanda zote saba nchi nzima.
Waziri Bashe amesema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya ufunguzi Agosti 1, 2024 ambapo Maonesho hayo yanafanyika Kitaifa jijini Dodoma.
Aidha, Waziri Bashe amewakaribisha wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika Maonesho hayo katika Kanda zote ili kuweza kujifunza teknolojia mbalimbali zitazowanufaisha wakulima na wazalisha wa bidhaa za kilimo.
Maonesho ya Nane Nane 2024 yatakuwa katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye Uwanja wa John Mwakangale; Kanda ya Mashariki mjini Morogoro kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere; Kanda ya Kusini mjini Lindi kwenye Viwanja vya Ngongo; Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza katika Viwanja vya Nyamhongolo; Kanda ya Ziwa Mashariki mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi; Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kwenye Viwanja vya Themi; na Kanda ya Magharibi mjini Tabora kwenye Viwanja vya Fatma Mwasa.
Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024 ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ni miongoni mwa Halmashauri zitakazoshiriki kwenye maonesho hayo ya Nane Nane, kwa ngazi ya Mkoa na Kanda. Kwa ngazi ya Mkoa, maonenesho hayo yatafanyika Manispaa ya Songea Mtaa wa Sinai na kanda yatafanyika katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye Uwanja wa John Mwakangale. Halmashuri ya Wilaya ya Songea, wao wamejikita sana kwenye kilimo, mifugo na uvuvi
Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Bi Hellen Semzigwa amewakaribisha wananchi kutembelea mabanda ya halmashauriya Wilaya ya Songea, ili kujifunza teknolojia mpya ya kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji na kufanya kilimo cha kibiashara”
Mhe. Bashe aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli; Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Prof. Riziki Shemdoe; Menejimenti za Wizara ya Kilimo; na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Singida.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa