• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

Baraza la makanisa ya Kipentekoste Tanzania Mkoa wa Ruvuma latoa vifaa vya kupambana na corona

Tarehe ya Kuwekwa: June 4th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amepokea msaada wa Vifaa vya kupambana na Corona vyenye thamani ya sh.  milioni  1.5 kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) Mkoa wa Ruvuma.

Hafla  ya kukabidhi vifaa hivyo imefanyika leo katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea na kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa  CPCT.

Mndeme amelishukuru Baraza la CPCT Mkoa wa Ruvuma kwa msaada huo ambao amesema tangu Ugonjwa huo uingie mkoani Ruvuma,ni mara ya kwanza kupokea msaada kutoka kwenye madhehebu ya Dini.

Hata hivyo Mndeme amewaomba Viongozi wa Dini  kuendelea kumuomba Mungu na Kumshukuru kwa Neema zake ili Taifa la Tanzania liendelee kuwa salama dhidi ya corona.

Mndeme amesema hadi kufikia Mei 4,mwaka huu katika  Mkoa wa Ruvuma kwenye vituo nane vya kulaza wagonjwa wa corona, hakuna Mgonjwa hata  mmoja na kwamba Mkoa upo salama ambapo ametoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kufanya maombi ili ugonjwa huo uweze kutokomezwa nchini na duniani kote.

 ‘’Mimi niendelee kuwaomba sana viongozi wa dini, kwa majitoleo yenu kwa watanzania, na  kuliombea Taifa Letu na Rais wetu anaendelea kutuhimiza kuchukua Tahadhari,na mimi nachukua fursa hii kuwaahidi  vifaa hivi vitatumika  kwa malengo kusudiwa’’. Alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Mkoa wa Ruvuma Mchungaji Andrew Kyando amevitaja vifaa ambavyo CPCT wamevitoa kuwa ni ndoo kumi za kunawia mikono na sabuni za maji 30.

Vifaa vingine ni mashine tano za kunawa  maji ambazo zinatumika bila kugusa kwa ajili ya usalama zaidi,kipima joto la mwili kimoja(Thermal scanner) ambapo amesema vifaa vyote vimegharimu shilingi milioni 1.5.

Amesema CPTC inaunga mkono juhudi za serikali katika vita ya corona na kwamba inatambua umuhimu wa kutoa msaada huo ili wananchi wa Mkoa wa Ruvuma waendelee kujikinga na  wawe salama dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Naye Katibu wa Baraza la CPCT  Mchungaji Elimu Mwenzegule amemchukuru Mkuu wa  Mkoa wa Ruvuma  kwa kuwashirikisha Maaskofu,Wachungaji tangu ulipoingia ugonjwa hatari wa Corona Nchini.

Mchungaji Mwenzegule  amesema anamshukuru Mungu kwa kusikiliza maombi ya watanzania ambapo hivi sasa maambukizi ya corona nchini yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Baraza la makanista ya kipentekoste Tanzania linajumuisha umoja wa makanisa ya kilokole zaidi ya  80 yalipo nchini.

Imeandikwa na Jacquelen Clavery

Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Songea

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa