Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Songea, tarehe 12/02/2024, limepitisha Rasimu ya Mpango Na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa mwaka 2024/2025.
Baraza hilo lilioongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhe. Simon Kapinga Ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 inakasimia kukusanya na kutumia kiasi cha TZS 28,766,811,612.00.
Rasimu ya mpango na Bajeti hiyo iliwasilishwa na Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Ngd. Athuman Nyange, ambapo pamoja na mambo mengine alisema
“Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kwa mwaka wa fedha 2024/2025 inakasimia kukusanya na kutumia kiasi cha TZS 28,395,124,804.00 ikiwa TZS 16,127,854,000 ni Mishahara, TZS 1,120,508,000.00 ni fedha kwa ajili ya matumizi mengine kutoka serikali kuu (OC), Tshs 8,943,963,200.00 ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa “( Tshs 4,695,638,000.00 fedha za ndani ( Serikali kuu), Tshs 3,841,364,000.00 fedha za nje ( Wafadhili) na Tshs 397,679,996.00 fedha za utekelezaji wa maendeleo kutoka Mapato ya ndani ya halmashauri)”
Aidha Nyange ameeleza kuwa Bajeti hiyo imezingatia makundi ya msingi yalioainishwa kwenye nyaraka muhimu kama vile Dira ya Maendeleo ya Taifa, Mpango wa maendeleao wa Taifa kwa miaka mitano yaani 2021/2022 hadi 2025/2026, ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020, Sheria ya bajeti Sura namba 430 pamoja na kanuni zake, Mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa awamu ya tatu, Malengo ya Maendeleo endelevu ya 2030, maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mpango mkakati wa Halmashauri kwa kipindi cha miaka mitano 2020/2021 hadi 2025/2026 na Maelekezo mahususi ya mamlaka ya Serikali za mitaa yaliyomo katika mpango wa bajeti wa mwaka 2024/2025.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mhe. Simon Kapinga, alisema “ leo tumepitisha bajeti kwa ajili ya shughuli mbali mbali kama vile Mishahara ya wafanyakazi, Miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa Zahanati, Vituo vya Afya, Shule lakini pia utoaji wa mikopo ya asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa