Baraza la madiwa la Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma limepitisha kiasi cha shilingi bilioni 5.79 ambazo ni mapendekezo ya mpango wa bajeti ya matengezo ya barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA)kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Meneja wa TARURA Songea Mhandisi John Ambrose amefafanua kuwa fedha hizo zitatumika kujenga miundo mbinu ya barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 134 kupasua na kutengeneza barabara kwa matengenezo ya kawaida,maeneo korofi na muda maalumu pamoja na kujenga madaraja.
Mhandisi Ambrose ametaja vyavzo vya fedha hizo nikutoka kwenye Mfuko wa barabara,Mfuko wa jimbo fedha za maendeleo na fedha za tozo
.
Kwa upande wao baadhi ya madiwani wakitoa hoja na mapendekezo ya bajeti hiyo wameiomba Serikali kuongeza kiwango cha bajeti kwakuwa kiwango kinachopendekezwa hakikidhi mahitaji kutokana na sababu za kijiografia ya Halmashauri hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Menas Komba amehaidi kutoa ushirikiano wadhati kwa wakala wa barabara za Mijini na Vijijini katika kuhakikisha fedha za miradi zinafika na kazi iliyopangwa inafanyika ipasavyo ili wananchi waendelea kunufaika na barabara hizo.
Halmashauri ya wilaya songea inazaidi ya barabara 100 zinzonazosimamiwa na wakala wa barabara za Mijini na Vijijini nyingi zikiwa zimejengwa kwakiwango cha changarawe na udongo.
Imeandaliwa na kuandikwa
Jacquelen Clavery
Afisa Habari songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa