Asilimia 71 ya wakazi wa Songea wanatumia vyoo bora
JUMLA ya kaya 30,476 kati ya kaya 32,102 sawa na asilimia 71 katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wanatumia vyoo bora.
Mratibu wa Afya na Kinga wa Halmashauri hiyo John Kapitingana amesema kaya hizo zimebainika katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni 2019.
Kapitingana amesema Halmashauri imepanga hadi kufikia Desemba 2019 wanafikia lengo la asilimia 100 kwa kuhakikisha kaya zote ambazo bado hazijatembelewa,zinatembelewa na kuhamasishwa kujenga na kutumia vyoo bora.
“Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zipo katika kampeni ya afya na usafi wa mazingira kigezo kimojawapo kinachozingatiwa ni wananchi kuwa na vyoo bora na vinavyokidhi vigezo’’,alisisitiza.
Hata hivyo Mkazi wa kijiji cha Maposeni Kata ya Maposeni Magdalena Komba amesema Katika utekelezaji wa kampeni hiyo,wanaishukuru serikali kupitia Idara ya afya kwa kuwapa elimu ya matumizi ya vyoo bora aina ya sato ambavyo vinasifa ya kutumia maji kidogo,kuzuia harufu na wadudu kama inzi ambao ni wadudu hatarishi kwa afya ya binadamu.
Wananchi katika Halmashauri ya Songea wamechangamkia fursa hiyo kwa kuanza kujenga na kutumia vyoo hivyo ambavyo vinauzwa kwa gharama nafuu, kukinunua, ni rahisi katika usafishaji wake,havitoi harufu na vifaa zaidi kwa wananchi wanaoishi pembezoni
Jacquelen clavery
Kaimu Afisa Habari Songea DC
Juni 19,2019.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa