Meneja wa Wakala wa maji na Usafi wa Mazingira wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Mathias Pangras amesema asilimia 71 ya wakazi wa wilaya ya songea mkoani Ruvuma wanapata huduma ya maji safi.
Pangras amevitaja Vijiji ambavyo vinahuduma ya maji lakini siyotoshelezi kuwa ni Mpitimbi B, Mbingamharule,Matomondo,Matimira A na B,Mpangula,Matomondo, Mhukuru Lilahi na Mhukuru barabarani.
Katika hatua nyingi Pangras ameelezea mikamkati ya kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kuwa ni uchimbaji wa visima virefu na vifupi na kuendelea na usanifu katika Vijiji ambavyo havina huduma ya maji ya mtiririko.
Ametaja Vijiji ambavyo vimekosa huduma ya maji kuwa ni Makwaya Mbolongo,Mipeta,Nambendo,Magwamira Lusonga,Chiulungi,Nakawale,Kituro Lipokera,Maposeni,Morogoro,na vingine kuwa ni Mdunduwalo,Kizuka,Magagura,Mpandangindo,Lipaya,Mbilo,Parangu,Lyangwena naLitapwasi
Pangras amewarai wananchi kushirikiana na ruwasa kuibua vyanzo vya maji, badala ya kutegemea wataalam kufika maeneo ya vijijini kutafuta na kubaini vyanzo hivyo jambo ambalo litarahisisha utekelezaji wa miradi.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea inajumla ya vijiji 56 na wakazi wapatao 152,205 kati ya hao wakazi 103,172 wanapata huduma ya maji safi kutoka vyanzo mbalimbali vya maji ambavyo ni visima virefu na vifupi, chemichemi na mito.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa