TIMU YA HAMASA NA ELIMU KWA MPIGA KURA KUTOKA TUME HURU YA UCHAGUZI WAMEINGIA SONGEA DC
Timu ya Hamasa na utoaji elimu kwa wapigakura kutika tume huru ya Uchaguzi ya Taifa leo 07/01/2025 wamefika Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Timu hiyo ya hamasa ikiongozwa na Afisa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ndg. Hussein Makame imefika katika halmashauri ya Songea kwa lengo la kutoa Elimu ya mpiga kura kwa wananchi na mwisho kutoa hamasa kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza tarehe 12/1/2025 na kuhitimishwa tarehe 18/1/2025 ndani ya halmashauri ya wilaya ya Songea.
Timu hiyo imepokelewa na Afisa Mwandikishaji jimbo la Peramiho ambaye pia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi. Elizabeth M. Gumbo, ambapo watumishi wa halmashauri wamekua miongoni mwa waliohamasishwa kishiriki zoezi hili muhim la uboreshwaji wa Daftari la kudumu linalotegekea kuanza tarehe 12/01/2025 hadi 18/01/2025
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa