Afisa Mwandikishaji Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi. Elizabeth M. Gumbo amefunga semina ya mafunzo kwa maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata .
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza jana tarehe 5/1/2025 na kuhitimishwa leo tarehe 6/1/2025 katika ukumbi wa Halmashauri Lundusi.
Akifunga mafunzo hayo Afisa mwandikishaji jimbo la Peramiho amewasihi maafisa hao kutunza kiapo chao cha uaminifu na kuhakikisha wanatumia vyema ujuzi waliopata na kuwafundisha waandikishaji na BVR Operators ipasavyo ili kazi ifanikiwe.
Mwisho ametoa wito kwa maafisa hao kutoa hamasa kubwa kwa wananchi kujitokeza katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwanzia tarehe 12/1/2025.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa