Hospitali ya Taifa Muhimbili imehitimisha kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi wa kwa kuwafanyia uchunguzi na matibabu zaidi wananchi 405 ambapo kati yao 52 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa ya macho ikiwemo upasuaji wa kuondoa mtoto wa jicho.
Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Dkt. Geofrey Kihaule zaidi ya wananchi 27 wamepatiwa miwani kutokana na changamoto za uoni, wengine wamepatiwa matibabu ya kawaida ya macho na mmoja amepatiwa rufaa ya ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Dkt. Kihaule ameongeza kuwa pamoja na uchunguzi na matibabu hayo wataalam wa hospitali ya Mtakatifu Joseph wamepata fursa ya kujengewa uwezo na wabobezi hao kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma za matibabu ya magonjwa macho katika hospitali hiyo kwa manufaa ya wananchi.
“Napenda kuupongeza uongozi wa Muhimbili kwa kuona umuhimu wa kuwaleta madaktari hawa kutoa huduma katika Halmashauri yetu, uamuzi huu umewapunguzia wakazi wa Songea na maeneo ya jirani umbali na gharama za kwenda Dar es Salaam (Muhimbili) kupata matibabu haya” ameongeza Dkt. Kihaule
Kwa upande wake mwananchi aliyehudumiwa katika kambi hiyo ameishukuru serikali kwa kuwajali wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songe na kuomba utaratibu huo uendelee na kuongeza wigo wa huduma za ubingwa bobezi kwakuwa huduma hizo zinahitajika kwa kiwango kikubwa na wakazi wa Songea.
Hospitali ya Taifa Muhimbili imefanya kambi maalum ya ubingwa bobezi ya uchunguzi na matibabu ya macho Halmashauri ya Wilaya ya Songea, uchunguzi na matibabu yamefanyika katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph kwa muda wa siku nne kuanzia Desemba 26 hadi 29, 2024.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa