Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea, wakishirikiana na wataalam kutoka Kitengo cha Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Songea jana 04.01. 2025 walitembelea Kituo cha kulelea watoto wanaotoka katika mazingira magumu maarufu kwa jina la Makao ya watoto Chipole kinachopatikana kata ya Magagura Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Lengo la ziara hiyo ikiwa ni kuendelea kuwapa tabasamu watoto hao kwa kuwapatia zawadi mbalimbali za sikukuu.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Wilaya ya Songea na Timu ya Wataalam waliombatana nao, Ndg. Adam Mlele ambaye ni Afisa Tawala amesema
“zoezi hilo limelenga kuwapa furaha watoto wetu katika kipindi hiki cha sikukuu ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono na utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”
Zoezi hili limeratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea wakishirikiana na ofisi ya Mkurugenzi Songea DC kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe- kitengo cha Ustawi wa Jamii
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa