Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea Ndg. Mtela Mwampamba, amewaagiza watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule wote kuhakikisha kwamba kila Mzazi anachangia gharama za chakula ili kumhakikishia mototo kupata chakula lakin pia kuwa na Lishe Bora.
Ndg. Mwampamba ameyasema hayo katika kikao cha Kamati ya Lishe kwa robo ya tatu, kwa mwakaa Fedha 2023/2024, kikao hicho kilichofanyoika katika ukumbi wa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ambapo katibu tawala aliongoza kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya
Kikao hicho ambacho huratibiwa na Divisheni ya Afya, kwa kuambatata na wataalam wengine, ikiwemo watendaji wa kata zote 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
“ Kama tulivyokubaliana ndugu zangu, kwenye maadhimio yetu. Azimio la kwanza ilikua lazima watendaji wa Kata na Kijiji wahakikishe kwamba wazazi wote wanachanga chakula kwa ajili ya watoto. Hivyo watendaji waendelee na msimamo huu huu kuhakikisha kila mzazi amechanga”
“ elimu ya lishe bora na ulaji unaofaa indeekuolewa kwa jamii kupitia Mikutano yote ya Hadhara, Makongamano, Semina na Mashuleni pamoja na umuhimu wa kufanya mazoezi kwa jamii yetu yote. Mtela Mwampamba Katibu Tawala Wilaya ya Songea
Aidha Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Songea Dr. Geofrey Kihaule katika kusisitiza umuhimu wa lishe alisema
“ Pamoja na hayo tuhakikishe tunafanya tathmini ya hali ya lishe mara kwa mara ili kutokomeza maadui wa Lishe ambao ni Udumavu, Ukondefu, uzito uliozidi, Uzito pungufu na Utapiamlo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa