Katibu Mkuu wa Jumuia ya Umoja wa Wanawake Tanzania Dr Philis Nyimbi amewapongeza wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma kwa utekeleza mzuri wa ilani ya chama cha Mapinduzi kwa kusimamia vema fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dr Nyimbi ametoa pongezi hizo katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika Halmashauri hiyo na kuzungumza na wanachi kupitia mikutano ya hadhara katika Kata ya Parangu na Maposeni.
Dr Nyimbi amesema Ilani ya ccm katika wilaya ya songea inasimamiwa na kutekelezwa kwa viwango vinavyokubalika hivyo ,usimamizi wa fedha zinazotelewa na serikali kwa ajilia ya ujenzi wa miradi uendelee kusimamiwa vizuri na kutatua kero za wananchi.
“Kwadhati ya moyo wangu nimefurahishwa sana na utekelezaji wa Ilani ya CCM”,amesma Dr Nyimbi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mhe. Jenista Mhagama amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwakuendelea kutoa pesa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Jimbo la Peramiho.
Mhe. Mhagama amesema mageuzi katika sekta mbalimbali yanaendelea kufanyika kwa lengo la kuwasaidi wanachi kutatua changamoto zao na kujikwamua kiuchumi kunako chagizwa na upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme ambapo huduma hiyo kwasasa inapatikana kwa asilimia 80 na zoezi linalo endelea ni kufikisha huduma hiyo kwenye Vitongoji,ujenzi wa miundo mbinu ya barabara.
Ameitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa mradi mkubwa wa Shule ya Sekondari ya JENISTA MHAGAMA inayoendelea kujengwa katika Kijiji cha Parangu katika Kata ya Parangu ambao umepewa kiasi cha shilingi zaidi ya bilioni moja ambao unatarajia kufunguliwa mapema mwakani 2022 kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na hatima kitato cha tano hadi sita.
Akizungumzia sekta ya Afya amesema Serikali imetoa shilingi milioni 500 ambazo zimetokana na tozo kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya viwili ambavyo vinatarajiwa kujengwa Kata ya Kilagano na Liganga pamoja ujenzi wa uboreshaji wa vyumba vya kujifungulia akina mama katika Zahanati 10 ambazo ni Litowa,Mgazini,Kilagano,Ngahokora,Liula,Parangu,Muunganozomba,Kikunja,Lugagara na Peramiho(B)
Ameto wito kwa wanachi wa Jimbo la Peramiho kuendelea kuungamkono jitihada za Raisi kwa kufanyakazi kwa bidii na kuimarisha amani na utulivu.
Dr Nyimbi amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea akiwa na agenda ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ,Shukrani kwa wananchi kwa kukichagua Chama cha Mapinduzi kushika dola,Uhai wa Chama,Mahusiano na zoezi la Sensa ambalo linatarajia kufanyika mwaka 2022.
Katika ziara hiyo Dr Nyimbi ametembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa shule ya sekondari Jenista katika Kijiji cha Parangu shule ambayo kukamilika kwake itatatua changamoto za watoto wakike ambao wamekuwa wakikabiliwa na vikwazo mbalimbali kikiweno cha mimba za utotoni.
Imeandikwa na
Jacquele Clavery
Afisa Habari
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa