Bima ya Afya
Wananchi wanashauriwa kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa iliwaweze kupata huduma ya matibu hata pale wanapokosa za Pesa za kulipia huduma hiyo
Kauli hiyo imetolewa na mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya songea Dr Yesaya Mwasubira katika mafunzo ya siku tatu yakuwajengea uwezo waganga na wenye viti wa bodi za afya namna ya kuingiza taarifa kwenye mfumo, usimamizi wa fedha katika vituo vya kutolea huduma,usimamizi wa ununuzi wa madawa na jinsi ya kuwasilisha maombi kwa mzabuni yaliyo fanyika katika ukumbi wa emau mji mdogo wa Peramiho hivi karibuni.
Dr Mwasubira amesema mfuko wa bima ya afya ulioboreshwa Unalengo mahususi wa kutoa huduma bora kwa wananchi waliojiunga na mfuko huo kwa mwanachama kuchangia shilingi 30000 kwa mwaka ambapo mwanachama atatibiwa yeye na kaya yake kwa matibabu ambayo mwanachama anastahili kupata kulingana na vigezo vilivyowekwa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa