ZOEZI la uandikishaji wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza mwaka 2023 linaendelea katika shule zote zilizopo Songea vijijini.
Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea amesisitiza wazazi na walezi wote wenye watoto kuanzia miaka mitano 5 hadi 6 waweze kuwaandikisha shule.
Amesema zoezi la uandikishaji ifikapo tarehe 30/12/2022 itakuwa mwisho wa zoezi hilo, hivyo wazazi wajitahidi kwa muda huu uliobaki kuhakikisha wanawaandikisha watoto.
Aidha, ameongeza kuwa wazazi wawaandikishe watoto katika shule zilizopo karibu na maeneo wanayoishi.
“Elimu ni haki ya kila mtoto tuishiriki kuitekeleza”.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa