Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, ( Sera, Bunge na Uratibu) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama anategemea kuanza Ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Lengo la Ziara hiyo ikiwa ni kuzungumza na Wananchi wa Halmashauri ya Songea kuanzia tarehe 6/07/2024 hadi 15/07/2024. Mhe. Mbunge atatembelea wananchi katika kata zote zilizopo halmashauri ya Wilaya ya Songea.
" Mbunge wa Jimbo la Peramiho, atafayanya mikutano ya hadhara ( Kuongea na Wananchi) kukagua miradi katika kata na vijiji vilivyopo jimbo la Peramiho kwa muda wa siku kumi (10) amesema katibu wa Mbun ge Jimbo la Peramiho.
Ametoa wito kwa wananchi waliopo Jimboni hapo ( Peramiho) kuhudhuria Mikutano hiyo ili kupata fursa ya kusikia namna Mbunge anavyotatua Kero za Wananchi lakini pia wananchi kupata nafasi kuongea na Mbunge.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa