Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Simon Kapinga amewataka waheshimiwa madiwani kisimamia vyema fedha za miradi ambazo zimepelekwa katika kata zao ili ziweze kukamilisha miradi iliyokusudiwa.
Ameyasema hayo katika kikao cha robo cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Lundusi- Peramiho.
Aidha, Mheshimiwa Kapinga ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwenye Kata, Vijiji na Vitongoji.
Vilevile kwa nafasi ya kipekee ametoa shukurani kwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuendelea kupambana bega kwa bega na kuhakikisha kwamba changamoto mbalimbali ndani ya Kata zinaenda kupatiwa majibu.
“ Kwasasa hivi kazi yetu kubwa Waheshimiwa Madiwani ni kwenda kusimamia vizuri fedha ambazo zipo kwenye Kata zetu kuhakikisha kwamba miradi inakwenda kutekelezwa na kwa viwango vinavyokubalika “, amesema Mheshimiwa Kapinga.
Pia ametoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Neema Maghembe, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Idara ya fedha kwa kusimamia vizuri swala la ukusanyaji wa mapato na kutekeleza agizo la serikali la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na kwa watu wenye ulemavu ambayo itawasaidia kutimiza malengo waliyojiwekea.
Mheshimiwa Kapinga ameongeza kuwa kila mmoja asimame kwenye nafasi yake katika kutekeleza majukumu ili kuhakikisha Halmashauri inasonga mbele.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa