WAHESHIMIWA Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wamefanya Baraza la robo ya nne kwa mwaka ulioishia Juni 2023 tarehe 24/08/2023 katika ukumbi wa mikutano Lundusi-Peramiho.
Baraza hilo limeudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata, Wataalamu kutoka TAKUKURU, Usalama na Ofisi ya RAS.
Akizungumza Kaimu Mwenyekiti Mheshimiwa Simon Kapinga ambae ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri amewataka wataalamu kuendelea na zoezi la doria katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza mapato ambayo yatakwenda kukamilisha miradi iliyopo katika Kata na Vijiji na shughuli za maendeleo.
Sambamba na hilo Mhe. Kapinga amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kufanya mikutano ya hadhara yenye lengo la kuwahimiza wananchi kutunza mazao kwa ajili ya chakula.
“Bei ya mazao kwa sasa ipo juu hivyo Watendaji katika mikutano hiyo waambieni wananchi wasidanganyike na bei hizo wakapata tamaa ya kuuza chakula chote wajitahidi kutunza chakula kingine kwa ajili ya familia”, amesisitiza Mhe. Kapinga.
Vilevile Mheshimiwa Kapinga amesisitiza Idara za Elimu Msingi na Sekondari kufanya jitihada za makusudi kwa shule ambazo zina wanafunzi wa jinsia ya kike na kiume ambazo hazina walimu wa kike ziweze kupelekewa kwani itasaidia wanafunzi hao kuwa huru kuelezea changamoto zao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Bi Zawadi Nyoni amempongeza Mheshimwa Mwenyekiti kwa kuendesha kikao kwa weredi na ameahidi maelekezo yote yaliyotolewa ameyapokea kwa ajili ya kuyafanyia kazi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa