• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

WILAYA ya Songea yapata bilioni 1.2 kujenga miundombinu ya Elimu

Tarehe ya Kuwekwa: June 14th, 2021

 Serikali imetoa shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa,vyoo na ukamilishaji wa ujenzi wa maabara katika shule za sekondari na Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Nyange Athuman amesema fedha hizo tayari zimeingizwa kwenye akaunti za shule husika kwa ajili ya kazi ya ujenzi na ukamilishaji wa miradi iliyokusudiwa kutekelezwa kwenye shule hizo.

Nyange ametoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya fedha hizo kuwa ni milioni 210 zitatumika kukamilisha ukarabati wa maabara katika shule za sekondari saba ambazo kila shule zimepata mgao wa shilingi milioni 30, shilingi milioni 266,400,000 zitatumika kujenga vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za msingi na sekondari.

Amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 820 zitatumika kuendeleza ujenzi wa sekondari mpya ya wasichana ya Jenista inayojengwa katika Kata ya Parangu Kijiji cha Parangu

Ameongeza kwakusema  ujenzi wa vyumba vya madarasa utahusu shule tatu za sekondari zilibahatika kupata mgao ambapo shule ya Sekondari Nalima na Namihoro zimepata milioni 53,200 000 kila moja na shule ya sekondari Muhukuru imepata shilingi milioni 40.

Aidha kwa upande wa ujenzi wa matundu vyoo sekondari ya Nalima na Namihoro zimepata shilingi milioni 13,200,000 kwa kila shule.

 Amezitaja Shule za msingi ambazo zimepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarsa kuwa ni Magagura,Matama,Matimira, Mbinga mhalule ambapo kila shule imepata mgawo wa shilingi milioni 13,200,000.

Amesema shule za msingi Putire,Kilagano,Kizuka,Matimira  na Mbinga mhalule zimepata fedha toka Serikali kuu za EP4 kwa ajilii ya ujenzi wa matundu sita ya vyoo kwa kila moja na vyumba viwili vya madarasa kwa kila shule.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Sekondari  wa Halmashauri hiyo Bumi Kasege amezitaja shule saba kati ya 16 za Serikali zilizo pewa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara kuwa ni shule ya Sekondari Namihoro, Darajambili, Lupunga,Matimira,Muhukuru,Muhukuru barabarani na Liganga ambapo kila shule imepata shilingi milioni 30.

Kasege amesema ukarabati wa kukamilisha maabara hizo umeanza tangu juni mosi mwaka huu na unatarajia kukamilika ifikapo juni 30 mwaka huu kulinga na miongozo na makubaliano ya fundi kiongozi aliyepata dhamana ya kazi hiyo

“Nimefuatilia kazi hiyo kwakufika kwenye shule hizo na kubaini hali ya ujenzi inanyoenda vizuri hadi juni 30 na tegemea kazi itakuwa imekamikika”, alisisitiza kasege.

Akizungumza kwaniaba ya mafundi viongozi Tito Mwenda ambaye anakamilisha ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari Muhukuru amesema wanauhakika wa kukamilisha kazi kwa wakati kwasababu hakuna changamoto itakayokwamisha na vifaa vyote vinavyohitajika vimenunuliwa.

Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma inajumla ya shule za Sekondari 21 kati ya hizo 16 ni za Serikali na zinazo milikiwa na watu binafsi ni tano,shule za Msingi ni 75 za Serikali ni 73 na zinazomilikiwa watu binafsi ni mbili.

Imeandikwa na

Jacquelen Clavery

Afisa Habari Songea DC

14 /06/2021

Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa