Halmashauri ya wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imeingia mkataba na kampuni ya West Food Comp LTD ya kutoka Makambako Mkoani Njombe kwa ajili ya kukusanya ushuru wa mazao.
Makubaliano ya mkataba huo yamefanyika leo katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwekeana saini baina ya Mkurugenzi wa Kampuni na Uongozi wa Halmashauri.
Akisaini mkataba huo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Tanu Kameka ametoa wito kwa Kampuni kufanya kazi waliyoomba kwa ufanisi kwasababu Serikali inategemea mapato kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.
Mweka hazina wa Halmashauri hiyo Rajabu Lingoni amesema katika kuboresha ukusanyaji wa mapato vikao vya kisheria vilikubaliana kumpata mzabuni atakayefanya kazi ya ukusanyaji wa ushuru wa mazao baladala ya kuendelea kuwatumia mawakala.
“Utaratibu wa kutumia zabuni katika kukusanya ushuru wa mazao utadhibiti mapato” Amesema lingoni.
Amesema maamuzi ya kumtumia mzabuni ni jambo nzuri litakalo saidia kudhibiti mapato ya Halmashauri,maamuzi hayo yamefikia baada ya kubaini unaudanganyi mkubwa katika ukusanyaji wa ushuru,unaofanywa na baadhi wa Tendaji wa Kata kupitia mawakala wao kitendo ambacho kilikuwa kinakwamisha jitihada za Halmashauri katika kutekeleza majukumu yake.
Lingoni amesema jumla ya vizuio 15 vimeanishwa na vimekabidhiwa kwa mzabuni ambavyo vitatumika katika kukusanya ushuru wa mazao kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Machi 2021hadi Machi 2022.
Lingoni amesema mzabuni anatakiwa kukusanya ushuru kwa kuzingatia taratibu,kanuni na sheria za ukusanyaji wa mapato zilizowekwa na Serikali na Halmashauri pasipo kumbughuzi mtu yeyote na Ofisi ya Mkurugenzi itafanya shughuli ya usimamizi na ufuatiliaji katika zoezi hilo.
Kwa upande wake mhasibu wa mapato wa Halmashauri hiyo Noel Chengula amepongeza utaratibu wa kutoa zabuni katika kazi ya ukusanyaji ushuru ni kitendo kinachoonekana kitaongeza ufanisi na kuondoa usumbufu na gharama za kuwalipa mawakala ambao awali walikabidhiwa jukumu hilo.
Chengula amesema sambamba na kuongeza ufanisi jambo hilo litasaidi kupunguza changamoto ya madeni kwa baadhi ya Watendaji wa Kata na Vijiji na mawakala,gharama za ufuatiliaji,na fedha kufikishwa bank kwa wakati
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni hiyo Godwin Chengula amehaidi kufanyakazi kwa ufanisi kwa sababu ni mzoefu katika kazi ya ukusanyaji ushuru ,na anafanyakazi hiyo katika maeneo ya Wilaya ya Ulanga ,Ifakara ,Makambako na Manispaa ya Songea
Imetaarishwa na kuandikwa na,
Jacquelen Clavery ,
Afisa Habari
Songeadc.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa