Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh kassimu Majaliwa amebariki zahanati 4 kuwa vituo vya afya
Mhe Majaliwa amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kilagano kijiji cha Lugagara Songea vijijni wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni Wilayani humo.
Mh Majaliwa ametoa kauli hiyo kufuati ombi la Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira, Kaz,i Vijana na Walemavu Mh Jenista Mhagama kuomba zahanati 4 zipandiswe hadhi kuwa vituo vya afya kwasababu zinakidhi vigezo.
Waziri Mkuu amewataka wananchi kwa kushirikiana na Halmashauri kuongeza,kujenga nyumba moja ya mtumishi wa afya atakaye toa huduma katika vituo hivyo na chumba cha kuhifadhia maiti
Zahanati ambazo zimepewa hadhi ya kuwa vituo vya afya ni Lugagara,Nakahegwa, Mpingi na Lipaya ambazo zitatoa huduma za upasuaji,mama na mtoto maabara, huduma ya kuhifadhi maiti na matibabu ya nje.
Aidha Waziri Mkuu ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuanza mara moja ujenzi wa hospitali ya Wilaya kwasababu serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni moja na nusu kwa ajili ya ujenzi huu,hata hivyo Halmashauri hiyo imeshaanza maandalizi kwa kutenga eneo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 70 katika kata ya Mpitimbi ,kijiji cha Mpitimbi (b) ambako hosiptali hiyo itajengwa.
Amewata wananchi kuendelea kujenga zahati kwa vijiji ambavyo havina zahanati na serikali itatoa vifaa vya viwandani na watumishi
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa