Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kassim majaliwa, ameziagiza mamlaka za mikoa na serikali za mitaa kuhakikisha wanatenga bajeti, kwa ajili ya kuibua,kutangaza na kuhifadhi maeneo yote ya kihistoria.
Maagizo hayo,yametolewa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Inocent Bashungwa kwa niaba ya waziri Mkuu, wakati akifunga Tamasha la kumbukizi la Vita vya majimaji na Utalii wa kiutamaduni, lililofanyika leo katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya majimaji Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma .
Waziri Mkuu Majaliwa ameziagiza mamlaka za Mikoa na Serikali za mitaa kutenga bajeti ,kwa ajili ya kuhakikisha maeneo yote ya kihistoria ya kiutamaduni yanatambuliwa na yanahifadhiwa kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.
Ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kuendelea kuadhimisha kumbukumbu ya maadhimisho ya Mashujaa, kila mwaka ili kuhifadhi Historia ya nchi na Ukombozi wa kusini mwa Bara la Afrika.
Ameongeza Wizara zote mbili zihamasishe jamii na kuelimisha kuwa, wanayofursa ya kumiliki maeneo ya Malikale na kuanzisha makumbusho kama sera ya malikale ya mwaka 2008 inavyofafanua.
“Mashujaa babu zetu wamepigana kwa ajili ya Taifa kilichobaki ni kwetu Vijana kutimiza wajibu, kupitia Vita vya majimaji ambavyo wazee wetu walipigania Uhuru, kwa kutumia mbinu mbalimbali, walipanda mbegu ya kizalendo, vinatukumbusha ni kitendo cha kizalendo kwa kuipenda Nchi yetu kwa kushirikiana, kushikamana wakaweza kuikomboa Tanzania” amesema Majaliwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Cosmas Nshenyi amesisitiza Suala la Uzalendo kwa kuandaa taifa la kizalendo, ambalo litakuwa na jukumu la kusimamia na kuhifadhi historia ya Nchi na Utamaduni, wa Mtanzania kwa kuijali na Kuipenda Tanzania.
Naye Chifu wa kabila la wangoni Ema Nkosi wa Mamkos Emanueli Zulu Gama ameiomba Serikali kufanya mchakato wa kuipandisha hadhi, Makumbusho ya Taifa ya Majimaji kuwa makumbusho ya kwanza kusini mwa bara la Afrika, kwa kuwa makumbusho haya ya majimaji yamekuwa yanatoa fursa ya kushikiana na Nchi nyingine za kusini mwa Bara la Afrika katika kufanikisha Tamasha la Kiutamaduni.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Taifa Dr Noel Lwoga, amesema Makumbusho ni Taasisi ya Kielimu ambayo ina jukumu la kukusanya, kutafiti na kuhifadhi na kuelimisha jamii kuhusu urithi wa Taifa letu, hivyo linawajibu Mkubwa katika kufundisha na kuelimisha jamii kuhusu Historia ya Tanzania kwa Vitendo kupitia Tamasha la Kiutamaduni, na kukuza Utalii wa ndani wa kiutamaduni.
Aidha Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na Utalii christowaja Ntandu, amesema Wizara inamikakati ya kutangaza maeneo muhimu ya Kihistoria ya Viongozi wetu wa jadi, ya wapigania Uhuru na yale yenye historia ya Nyerere katika Mkoa wa Ruvuma na mikoa mingine Tanzania. Lengo ni kuyahifadhi na kuyaendeleza kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Utalii.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa