Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho ametoa rai kwa wawekezaji mbalimbali katika jimbo la Peramiho kuendelea Kufanya uwekezaji wenye tija kwa wananchi, kwa Halmashauri na kwa Taifa.
Hayo ameyasema wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Muhukuru katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Songea leo tarehe 12/07/2023.
“Tunataka wawekezaji wajue wana wajibu wa kuchangia shughuli za maendeleo kwenye vijiji vinavozunguka maeneo uwekezaji,” alisisitiza.
Makaa ya mawe yamekuwa bidhaa muhimu na adhimu, uwekezaji umeendelea kukua na masoko yameongezeka, wawekezaji waangalie ajira zile zinazosaidia kuendesha miradi yao ili kutoa kipaombele katika maeneo ya vijjiji vilivyozunguka mradi, alisema Waziri Mhagama.
“Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan amefanya kazi nzuri ya kuvutia Wawekezaji Mbalimbali, Wawekezaji wa shamba la Miwa, Wawekezaji wa Makaa ya Mawe, na Wawekezaji wa Umeme wa Maji, naomba kila Muwekezaji aliyeomba ardhi ya uwekezaji atumie kama alivyoomba,”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mhe. Menas Komba amesema uwekezaji wa Makaa ya Mawe kuna mpango kabambe ambao umelenga kupata asilimia moja ya kila awamu ya mauzo.
“Tuendele kushirikiana na wawekezaji wanaokuja kuwekeza ili waendelee kutusaidia na Halmashauri itasimamia kupata haki za wananchi” alisema Mhe. Komba
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Mwalimu Neema Maghembe amesema wawekezaji wote waliowekeza katika Halmashauri ya Songea wamefuata taratibu zote za uwekezaji.
“Tunawawekezaji wa kutosha, wengine wanaendelea na kazi za tafiti mbalimbali na wengine wako katika hatua ya kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe”, alisema Ndugu Maghembe
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa