Watanzania asilimia 5 wanamaambukizi.
Asilimia 5 ya watanzania wote wameambukizwa UKIMWI na asilimia 95 hawajaambukizwa kulingana na utafiti wa 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vinajana,Ajira na Walemavu Mhe Jenista Mhagama amesema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi magari ya mradi wa mwitikio wa kuthibiti UKIMWI kwa Mikoa ya Nyanda za juu kusini iliyofanyika mjini songea hivi karibuni.
Mhe Mhagama amesema Watanzania asilimia 5 wameambukizwa ukimwi na asilimia 95 hawajaambukizwa kulinga na utafiti wa 2017 na Serikali itahakikisha wanapatiwa huduma zinazotakiwa pamoja na dawa za kufubaza virusi vya UKIMWi na lishe,na asilimia 95 wasio ambukizwa wanalindwa kwa kupewa elimu kwa njia mbalimbali.
Kutokana na utafiti wa 2016/ 2017 kuhusu maambukizi dhidi ya ukimwi Nchini,Mikoa ya Nyanda za juu kusini ilionekana kuwa na tatizo la maambukizi yakuwa juu au sawa na wastani wa kitaifa ambao ni asilimia 4.7 sababu iliyopelekea kuunda mkakati wa uratibu wa mradi wa mwitikio wa kudhibiti UKIMWI kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini.
Ugonjwa wa UKIMWI upo Nchini takribani miaka 30 mpaka sasa,na Watanzania zaidi ya milioni moja wanatumia dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI,na mkakati wa Serikali kupunguza maambukizi mapya hadi kufikia asilimia 0.3 hadi kufikia 2030 kutoka 4.7 ya saasa na tatizo la UKIMWI bado lipo hivyo kila mtu anatakiwa kuwa makini kujilinda dhidi ya maambukizi mapya ya VVU.
Jacquelen Clavery -TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa