TIMU ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakiongozwa na Afisa Elimu Msingi Daniel Ngongi wametembelea na kukagua miradi inayotekelezwa katika Halmashauri.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na miradi ya SWASH inayotekelezwa katika shule ya Lung’oo matundu 14 ya vyoo unaogharimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 36.1 Lihuhu matundu 13 unagharimu kiasi cha shilingi milioni 33.7 Makambi matundu 13 unagharimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 34.2 na Parangu matundu 15 yanayogharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 37.6.
Vilevile wamekagua miradi ya BOOST inayotekelezwa katika shule ya msingi Kizuka ujenzi wa madarasa mawili unagharimu fedha kiasi cha shilingi Milioni 53.1 Ngahokora mradi wa ujenzi wa madarasa mawili unaogharimu fedha kiasi cha milioni 53.1 na madarasa mawili ya Awali ya mfano milioni 55.8 shule ya msingi pamoja na Matama fedha kiasi cha shilingi milioni 53.1.
Pia wametembelea miradi ya ujenzi wa vituo vya Walimu ( TRC) vilivyopo katika Kata ya Mpitimbi ambacho kinagharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 22 na Peramiho milioni 22.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa