Wanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wakiongozwa na Wakili msomi Pascal Kapinga, wamefanya ziara katika kata mbalimbali zilizoko halmashauri ya Songea, na kukutana na Mabaraza ya Kata, lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo ili waweze kutenda haki katika majukumu yao.
Akizungumza katika utangulizi wa Semina hiyo wakili msomi Hussein Hamidu amesema “tumekuja kuwakumbusha na kuwaelewesha kuusu namna ya utatuaji wa migogoro ya Ardhi na migogoro mingine katika kata zenu, lakini pia pamoja na mambo mengine kuja kuwaeliisha kuhusu mabadiliko ya sheria mpya ambayo yamefanyiwa marekebisha mwaka 2021, ambayo yanalenga namna ya kutatua migogoro ya ardhi kwa njia ya usuluhishi.
Aidha Mr. Hussein aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu mpango wa Serikali katika kuhakikisha wananchi wake wanaondokana na migogoro, hivyo kuweka mikakati thabiti ya kupunguza migogoro ya Ardhi kwa kuweka mifumo mizuri na kuboresha sheria za Ardhi
Katika kutatua changamoto zinazoukabili Mfumo wa utatuzi wa migogoro ya Ardhi, Serikali imechukua hatua Mbalimbali ambazo zimelenga kuboresha mfumo wa utoaji haki hususani kutatua migogoro ya ardhi.
Hatua zilizochukuliwa na serikali ni pamoja na kuanzisha sera ya Taifa ya Ardhi ambayo inaelekezwa uanzishwaji wa mfumo wa utatuzi wa mgogoro ya Ardhi ambao ni wa haraka, huru na unaofikika. Serikali pia imetunga Sheria ya Ardhi Sura 113, Sheria ya Ardhi vijiji Sura 114 pamoja na Sheria ya Mahakama za Ardhi Sura 216. Sheria hizi pamoja na maswala mengine zimeweka mifumo ya utatuzi wa migogoro ya Ardhi ili kufikia malengo ya Sera ya Taifa ya Ardhi.
Ofisi ya Rais, TAMISEMI inatarajia kuwa Mwongozo huu utasaidia Mabaraza ya Kata Tanzania Bara katika utekelezaji majukumu yake ya usuluhishi wa migogoro ya Ardhi na kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa haraka, wakati na kwa urahisi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa