Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari Ya kusombwa na maji
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amewataka wanachi wa Halmashuri ya Wilaya Songea Mkoani Ruvuma kuchukua tahadhari ya kusombwa na maji kufuatia baadhi ya mito kufurika maji.
Mgema ametoa tahadhari hiyo wakati akikagua majaraja na barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma hivi karibuni
Amewataka wananchi kuchukua tahadhari yakusombwa na maji na kusubiri wanapokuta mto umefurika maji kwasababu wanaweza kusombwa na maji na kusababisha madhara ya kibinadamu.
Amesema mvua zinazoendelea kunyesha zinasababisha baadhi mito mingi kufurika nakuleta adha kwa wananchi ikiwemo uchakavu wa miundo mbinu ya barabara na madaraja katika maeneo mbalimbali
Mgema amewaka Wakala wa Barabara wa Mijini na Vijiji pamoja na Wakala wa Barabara kufanya matengezo katika maeneo ambayo yanaonekana kuleta adha kwa wanachi kwa kipindi hiki cha masika.
Aidha amewaonya wananchi kutofanya shughuli zakibinadamu kamavile kilimo na malisho ya wanyama umbaliwa wa mita 60 kutoka kwenye kingo za mto kwa sabababu shughuli hizo zinasababisha mito kuboa kingo maji kukosa mwelekeo na kusambaa ovyo.
Baadhi ya wananchi wameomba serikali kuwajengea madaraja ambayo yamakuwa kikwazo kwao katika kutekeleza majukumu yao na uptikaji wa huduma za kijamii kutoka eneo moja kwenda jingine pindi daraja linaposombwa na maji hasa kwakipindi cha masika.
Mgema alitembelea eneo la Mto Njoka,daraja la Mhukuru linalounganisha na kijij cha Matama,daraja la linalounganisha Nchi ya Tanzania na Msumbiji Mkenda Ofisi za Uhamiaji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji ambapo eneo hilo nalo lilifurika maji nakusababisha changamoto kwa wasafiri pamoja na nyumba moja ya mwananchi kusombwa na maji.
JACQUELEN CLAVERY
K/AFISA HABARI SONGEA DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa