• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Songea District Council
Songea District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Uongozi
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
  • Utawala
    • Eneo la Utawala
    • Braza la Madiwani
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
        • Maliasili
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo na Umwagiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ardhi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Internal Auditor
      • TEHAMA
      • TASAF
      • Ugavi na Manunuzi
      • Usafi Mazingira na Taka ngumu
      • Mawasiliano Serikalini
      • Maendeleo ya Miundombinu Mjini na Vijijini
      • Mawasiliano Serikalini
      • Sheria
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Albam ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi ya Afya
    • Boost
    • Swash
  • Madiwani
  • Tarafa
  • Fursa za Uwekezaji
  • Shule
    • Shule za Msingi
    • Shule za Sekondari

WANANCHI waipongeza Serikali kupitia TARURA kujenga barabara ya lami Matomondo-Mlale.

Tarehe ya Kuwekwa: March 27th, 2023


BAADHI ya wakazi wa kata ya Mbinga Mhalule wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, wameipongeza Serikali kupitia wakala wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA),kwa kutekeleza vizuri ujenzi wa mradi wa barabara ya Matomondo-Mlale Jkt kwa kiwango cha lami.


Wamesema,TARURA ni mfano bora wa kuigwa kwa taasisi nyingine za umma katika kutekeleza na kusimamia miradi yake,na kuishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,kutatua kero ya mawasiliano kwa wakazi wa kata hiyo na makao makuu ya wilaya Songea mjini.


Clous Mpenda alisema,kujengwa kwa Barabara ya Matomondo-Mlale Jkt kwa kiwango cha lami itachochea kukua kwa uchumi wao kwa kusafirisha mazao wanayozalisha na kufanya shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato kati ya Mbinga Mhalule na maeneo mengine.

Alisema kabla ya kujengwa kwa kiwango cha lami,changamoto kubwa ilikuwa namna ya kusafirisha mazao kutoka shambani kwenda sokoni kutokana na ubovu wa barabara hiyo, jambo lililochangia umaskini mkubwa licha ya jitihada kubwa wanazofanya kujikwamua na umaskini kupitia shughuli zao za kilimo.

“kwanza tunaishukuru sana serikali  kupitia Rais wetu mpendwa Dk Samia Suluhu Hassan kutoa fedha zinazotumika kujenga barabara hii,pia tunawapongea  wataalam wote wa Tarura kwa usimamizi mzuri,hii barabara ni muhimu sana kwetu sisi”alisema Mpenda.

Mpenda ameiomba serikali,kuendelea kujenga kipande cha barabara kilichobaki kwa kiwango cha lami ili kurahisisha mawasiliano kati ya kata ya Mbinga Mhalule-Magagura na maeneo mengine ya wilaya ya Songea ambayo ni maarufu kwa kilimo cha zao la mahindi.

Christian Komba alisema,atatumia fursa ya barabara ya lami kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kuwaomba wananchi wenzake kuitunza barabara hiyo na kuitumia kuondokana na umaskini.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA wilaya ya Songea Mhandisi Bakari John alisema,ujenzi wa wa barabara ya Matomondo-Mlale Jkt yenye kilomita 21 kwa kiwango cha lami ulianza mwezi April mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika  Mwezi Machi 20233.

Alisema,barabara hiyo inajengwa kwa awamu mbili,na katika awamu ya kwanza imetekelezwa umbali wa kilomita 3.5 kwa gharama ya shilingi bilioni 4.

Alitaja kazi zilizofanyika katika awamu ya kwanza ni ujenzi wa lami kilomita 3.5,ujenzi wa madaraja makubwa 3,kujenga vivuko vidogo vya maji (makalavati)49,kujenga mifereji kilomita 2.5 na kufunga taa za barabarani.

Alisema,barabara hiyo ikikamilika itawasaidia wananchi wa vijiji vya Matomondo,Mlale,Magagura,Nakahegwa ambavyo ni maarufu kwa kilimo cha mahindi kusafirisha  mazao yao na bidhaa nyingine kwa urahisi.

Mhandisi Bakari,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ambazo zimesaidia kujengwa kwa barabara hiyo na kueleza kuwa, fedha zilizotumika zinatokana na tozo ya mafuta ambapo amewataka  wananchi kuitunza ili iweze kudumu kwa mrefu.


Matangazo

  • Tangazo la Kuitwa kwenye Usaili Julai 2022 June 22, 2022
  • TANGAZO LA FURSA ZA KAZI KATIKA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI (UNHCR) August 26, 2022
  • TANGAZO LA KAZI October 13, 2022
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021. December 18, 2020
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • KIKAO CHA MAAFISA HABARI KIMEMALIZIKA KWA KUWEKA MAKUBALIANO ENDELEVU KWA MASLAHI MAPANA YA NCHI

    May 24, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA, WANATEGEMEA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA NA UBINGWA BOBEZI KATIKA HOSPITALI YA HALMASHAURI SONGEA

    May 21, 2025
  • MKIMBIZA MBIO ZA MWENGE KITAIFA, AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    May 11, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SONGEA DC, LIMEMSHUKURU MHE. RAIS NA WAZIRI WA AFYA KWA KUIHESHIMISHA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA

    April 29, 2025
  • Ona Zote

Video

NGOMA YA LIZOMBE
Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
  • Tovuti ya Manispaa ya Songea
  • Tovuti ya Halmashauri ya Mji Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Mbinga
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Namtumbo
  • Tovuti ya Halmashauri ya Wilaya Tunduru
  • Tovuti ya Halmashauri ya Madaba
  • Tovuti ya Halmashauri ya Nyasa

Tovuti Muhimu

  • Utumishi wa umma
  • Baraza la mitihani la Taifa
  • National Website
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya ajira
  • Tovuti kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Maeneo

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Songea

    Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea

    Simu: 2602320 / 2602176

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa