Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Mhe. Komredi Odo Mwisho amewataka wananchi wa Kijiji cha Mpitimbi B kutumia fursa zilizopo kujiinua kiuchumi wakati akikagua mradi wa Shamba darasa la ukuzaji wa viumbe maji mnamo tarehe9 Octoba 2023 wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma katika Kijiji hicho cha Mpitimbi B Kata ya Mpitimbi
Akikagua ujenzi wa miundombinu hiyo ambayo ni mabwawa manne(4), chumba cha darasa la kujifunzia, vyoo matundu mawili na fensi, amesema kuwepo kwa mabwawa hayo katika Kijiji hicho kitasaidia kukuza kipato cha wananchi wa maeneo hayo pia pindi mradi huo utakapo kamilika afya za binadamu zitaimarika kutokana na samaki watakao patikana kupitia mradi huo. Ambapo amesema
" Niwapongeze sana kwa hatua hii mlioifikia nami nawambieni kupitia kukamilika kwa mradi huu hakika mtapata mafanikio makubwa na yatawafanya mkue kiuchumi tulizoea kupata samaki kutoka Ziwa Nyasa, Victoria hata Ziwa Tanganyika na bahari ya Hindi lakini sasa kupitia mradi huu mtaweza kula samaki wanaozalishwa Kijiji cha Mpitimbi hivyo hiyo kwenu ni kama fulsa ya kukua kiuchumi na hilo ndilo lengo la Raisi wetu mama yetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwani anakiu ya kuona kila Mtanzania ananufaika na matunda ya nchi yake"
Basi kipekee naomba nitumie fursa hii kumshukuru Mhe. Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa wananchi wa Kijiji cha Mpitimbi na kuamua kutoa fedha kwaajili ya Mradi huu ambao utaenda kuwanufaisha watu wengi sana endapo utatumika vizuri, vilevile nimshukuru Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Joakim Mhagama kwa juhudi zake katika Jimbo hili kwa kweli zinaonekana na zinazaa matunda, pia nashukuru kamati nzima ya siasa ya Mkoa wa Ruvuma kwa kumuunga mkono Raisi wetu katika kuhakikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa vyema na watu wote waliofanikisha mradi huu kuendelea na ujenzi.
Akiwasilisha taarifa ya mradi Mtendaji wa Kijiji cha Mpitimbi B Naomi Gerson amesema kwamba mradi huo ulipokea fedha kiasi cha shilingi 123,930,000 kutoka wizara ya mifugo na uvuvi kwa bajeti ya mwaka 2022/2023, ikiwa gharama za vifaa ni shilingi 104,700,000 na gharama za ufundi ni Shilingi 19,230,000 na kufanya jumla ya shilingi 123,930,000 na mradi huo unatarajiwa kugharimi jumla ya shilingi 127,000,000. Ikiwa kwa sasa mradi umefikia asilimia 97% ya ujenzi hivyo mradi upo kwenye hatua za ukamilishwaji.
Mradi huo utakapo kamilika utakuwa na mabwawa4 yenye ukubwa wa 30m x 20m x 1.5m, uzio 100m x 90m , darasa la mafunzo, stoo na choo ya matundu mawili. Pia bwawa moja linatarajiwa kuchukua vifaranga 10000 na kufanya jumla ya vifaranga 40000 kwa mabwawa yote manne.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa