Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge Ajira na wenye Ulemavu( Mbunge) Mhe.Jesta Mhagama amesma wananchi wa jimbo la peramiho mkoani Ruvuma kuendelea kufungua fursa za kiuchumi katika jimbo la peramiho
Mhe Mhagama ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ya siku moja katika kata za ndongosi,mpitimbi na litapwasi aliyoifanya hivi karibuni.
Mhe Mhagama amesema ataendelea kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo hilo ili wananchi waendelee kunufaika na fursa hizo kupitia miradi iliyojengwa ,inayojengwa na itakayojengwa.
Amezitaja baadhi ya fursa ambazo wananchi wa jimbo hilo wanaweza kunufaika nazo kuwa ni ujenzi wa hospitali ya wilaya ,iliyojengwa katika kata ya mpitimbi,miundo mbinu ya barabara,upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme ambayo inapatikana kwa asilimia 80 ndani ya jimbo hilo.
Amesema kuwepo kwa miradi hiyo ni fursa kwa wananchi kunufaika nafusa hizo kwa kuanzisha shughuli za kiuchumi kama vile kilimo ,ufugaji ufundi wa kutengeneza bidhaa mbalimbai kama kutengeneza madirisha na biashara ndogo ndogo.
“ Naomba muwe na subira hayawi hayawi yatakuwa “,amesema mhe. Mhagama
Amewarai wananchi kuwa na moyo wa uvumili pindi wanapokuwa na changamoto za kupata huduma za kijamii kwani serikali yao ni sikivu na inasikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi hatua kwa hatua kwakuzingtia sera na ilani ya chama.
Amewahaidi wananchi wa kijiji cha Nambendo kwachimbia kisima cha maji chenye urefu wa mita 170 hadi 180 ambacho kitafungwa tanki na kusambaza maji kijijini hapo mara baada ya wataalam wa maji kufanya upembuzi yakinifu.
Amemshukuru Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassani kwakutoa fedha ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali katika Jimbo la Permiho ambayo inakuwa chachu ya kuchochea uchumi wa wananchi kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo kwa shule za msingi na sekondari,Vituo vya afya ,barabara ,miradi ya maji na huduma nyingine za kijamii.
Kwa upande wao wananchi wa kata hizo wamemshukuru mbunge kwakuwaunga mkono katika kutekeleza maendeleo yao kwakuwachangia fedha na vifaa vya viwandani katika miradi ya ujenzi na ushauri ambao umekuwa sehemu ya mafanikio kwao.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea dc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa