Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea ikiongozwa na Mkuu wa Idara hiyo Bi. Hellen Shemzigwa imeendesha ziara ya mafunzo ya kilimo cha kahawa katika mashamba ya wakulima wa kata za Parangu na Kilagano kwa lengo la kuwajengea uwezo wakulima wapya kutoka Kata ya Ndongosi, Kitongoji cha Maleta.
Bi. Shemzigwa aliwataka wakulima hao kuzingatia kilimo cha kahawa akieleza kuwa ni zao la muda mrefu na la kudumu linaloweza kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja, jamii na Halmashauri kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa Maleta, Thomas Kapinga alishukuru kwa mafunzo hayo na kusema kupitia elimu waliyopata wanatarajia kuongeza tija katika uzalishaji wa kahawa.
Naye mkulima wa kahawa wa Kilagano, Bw. Xavery Komba, ametajwa kuwa mfano bora kwa jamii kutokana na jitihada zake za kuendeleza kilimo hicho, ambapo wananchi wengi wamekuwa wakijifunza kupitia shamba lake. Aidha, amotesha miche zaidi ya laki tano kwenye kitalu ili kuwasaidia wakulima wa kata hiyo kuanzisha AMCOS na kuacha kutegemea zao moja la mahindi.

Kwa upande mwingine, Halmashauri ya Wilaya ya Songea imejipanga kuadhimisha Siku ya Kahawa Duniani tarehe 4 Oktoba 2025 katika mashamba ya AVIV. Kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, kutafanyika mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya timu ya wakulima wa kahawa na Songea DC FC siku ya tarehe 3 Oktoba 2025
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa