WAJUMBE wa kamati ya Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wamefanya kikao cha maandalizi ya bajeti ya lishe kwa mwaka 2023/2024.
Akizungumza katika kikao hicho Afisa Lishe wa Wilaya Joyce Kamanga amesema Halmashauri imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuendelea kutengwa kwa shilingi elfu moja (1000) kwa kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano.
Aidha amesema kwa kushirikiana na Idara mtambuka wataendelea kuhamasisha jamii na vikundi kuhusu umuhimu wa kufuga wanyama wadogo wadogo, samaki pamoja na kilimo cha mbogamboga katika kaya na mashuleni ili kuhakikisha hali ya lishe inakwenda vizuri na kupunguza tatizo la utapiamlo.
‘’Sisi kama wataalamu wa lishe kwa kushirikiana na watoa huduma za afya katika vituo vyote tutashirikiana kutoa ushauri nasaha na lishe wakati wa kliniki hii yote ni kuhakikisha tunawajengea elimu wazazi na walezi juu matumizi na uandaaji wa vyakula vya lishe kwa watoto’’, amesisistiza Afisa lishe Joyce.
Pia ameongeza kuwa wamedhamiria kuwepo kwa mwezi wa afya na lishe ya mtoto na kuwepo kwa maadhimisho ya siku ya afya ya Lishe ya Kijiji katika kila robo mwaka.
Vilevile amesisitiza kuundwe kamati ya lishe ngazi za Kata kwaajili ya kuhamasisha mambo mbalimbali yanayohusiana na lishe na kutoa elimu juu ya umuhimu wa unyonyeshaji kwa watoto.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa